Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni sita
kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Pacco GEMS Limited, Bw. Mahendra
Bardiya katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari
wilayani Ruangwa ambapo jumla ya shilingi milioni 138.26 zilichangwa.
Harambee hiyo ilifanyika sambamba na mkutano wa hadhara uliohutubia wa
Waziri Mkuu mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akipokea cheti maalum cha kutambua mchango wake katika
kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa kutoka
kwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa katika mkutano wa
hadahara aliouhutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016.
(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti Maalum cha kutambua
mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi
wilayani Ruangwa alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi,
Ali Topa (kulia) katika mkutano wa hadhara aliouutubia mjini Ruangwa
Desemba 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa wilaya ya Ruangwam Issa
Njinjo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016.
(Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)





0 Comments