Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwa amewabeba watoto, Editha
(kushoto) na Edina wa Kituo cha kulea watoto yatima cha CHAKUWAMA
kilichopo Sinza jijini Dae es salaam jijini Dar es salaam wakati
alipotembelea kituo hicho na kutoa misaada mbalimbali. Desemba 24, 201.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
........................................................................................................
........................................................................................................
MKE
wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa makundi
ya watoto yatima jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha kufurahia sikukuu za
mwisho wa mwaka.
Mama
Majaliwa ametoa msaada huo leo (Jumamosi, Desemba 24, 2016) katika vituo vitatu vya CHAKUWAMA
kilichopo Sinza, HISANI kilichopo Kigamboni na CHAMAZI kilichopo Mbagala.
Akikabidhi
msaada huo ikiwemo mchele, sabuni, mbuzi, juisi na soda, Mama Majaliwa amesema
ameona ni vema atoe msaada huo kwa watoto hao ili na wao waweze kufurahia
sikukuu za mwisho wa mwaka kama ilivyo kwa watoto wengine.
Pia
ametoa wito kwa makundi mbalimbali yenye uwezo katika jamii wawe na moyo wa
kusaidia makundi yenye uhitaji.
Kwa upande wao, walezi wa vituo vya kulelea watoto
yatima vya CHAKUWAMA na HISANI wamemshukuru mke wa Waziri Mkuu kwa msaada huo
huku baadhi ya watoto wakisema msaada huo umewapa faraja kubwa.
Mlezi
wa kituo cha CHAKUWAMA, Bibi Saida Hassan mbali ya kushukuru kwa msaada huo,
amewaombea kwa Mwenyezi Mungu awape afya na nguvu za kuendelea kuwatumikia
vizuri Watanzania.
Naye
Mlezi wa kituo cha HISANI, Bi. Hidaya Mutalemwa ameiomba jamii iendelee
kuyakumbuka makundi yenye uhitaji kwani bado yanakabiliwa na changamoto nyingi za
kufanikisha ndoto zao ikiwemo kupata elimu.

0 Comments