Na Is-haka Omar,
Zanzibar.
MGOMBEA mteule wa
Tiketi ya CCM jimbo la Dimani Unguja, Juma Ali Juma amewashukuru na kuwapongezi viongozi wa ngazi zote za chama
hicho kwa jinsi walivyoendesha mchakato wa uteuzi wake.
Mteule huyo ambae
alitangazwa kati kati wa wiki hii baada ya kikao cha Kamati Maalum ya
halmashauri kuu ya CCM zanzibar alikuwa ni miongoni mwa makada 25 wa chama
hicho waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.
Akizungumza na Gazeti hili jana mgombea huyo alisema anavipongeza vikao hivyo vya CCM kwa kumuamini
kumpa jukumu la kupeperusha bendera ya Chama hicho katika Uchaguzi mdogo wa
jimbo hilo na kuahidi kutekeleza wajibu huo kikamilifu.
Alieleza kuwa katika
kutimiza wajibu huo kwa chama chake na wanancnhi kwa ujumla, atahakikisha
analinda, anaheshimu na kukiwakilisha vyema Chama chake katika uchaguzi huo.
“Chama Cha Mapinduzi kupitia watendaji,
viongozi, makada na wachama wake wote walioshirikiana kwa njia moja ama
nyingine kuanzia hatua za awali mpaka nateuliwa nawashukru sana kwa hekima na
busara zao hakika sitowaangusha popote nitakaposimama kunadi sera za chama na
serikali iliyopo madarakani.
Akizungumzia ushindani
katika mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama, Juma alisema ulikuwa mkubwa uliotawaliwa
na demokrasia, uhuru na maamuzi yaliyojaa busara.
“Ushindani uliokuwepo
katika uchaguzi wa ndani ya chama ni kipimo tosha cha kunifanya niamini kuwa
walioniteuwa wamejiridhisha kuwa nafaa kuvaa viatua vya alikuwa Mbunge wa jimbo
hili marehemu Tahir (Hafidh Ali).”, alieleza Juma.
Sambamba na hayo mteule
huyo aliweka wazi baadhi ya mambo atakayoyapigania ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha anasimamia utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020
kwa manufaa ya wananchi wa jimbo hilo
bila ya ubaguzi.
Jumla ya vyama viwili
Zanzibar vimetangaza nia ya kushiriki katika uchaguzi huo ambavyo ni Chama Cha
Wananchi (CUF) na CCM ambavyo vimekamilisha mchakato wa kumpata mgombea katika
uchaguzi huo unaofanyika baada ya kifo cha aliekuwa Mbunge wa jimbo hilo marehemu
Hafidh Ali Tahiri aliyefariki mwezi uliopita mjini Dodoma.

0 Comments