Mkuu wa mradi wa Agra, ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma, Dkt. Mark Msaki (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (Katikati) wakati akikagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 katika Mahafali ya 30 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza. Kushoto kwa Dkt. Kijaji na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula (Mb).
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Mwanafunzi wa kiume wa Stashahada Mwaka wa Pili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza, akielezea kuhusu mafunzo wanayoyapata chuoni hapo na namna elimu hiyo inavyosaidia kuendeleza vijiji walivyokwenda kufanya mazoezi kwa vitendo mkoani Mwanza, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (Hayupo pichani) alipotembelea na kukagua maonesho hayo ya taaluma, huduma na bidhaa zinazotolewa na chuo hicho.
Mwanafunzi wa kike wa Stashahada Mwaka wa Pili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza, akielezea kuhusu mafunzo wanayoyapata chuoni hapo na namna elimu hiyo inavyosaidia kuendeleza vijiji walivyokwenda kufanya mazoezi kwa vitendo mkoani Mwanza, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) alipotembelea na kukagua maonesho hayo ya taaluma, huduma na bidhaa zinazotolewa na chuo hicho.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akionesha moja ya machapisho yaliyotolewa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakati alipotembelea na kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 katika Mahafali ya 30 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkufunzi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Bw. Ezekiel Kanire, (aliyeshika kipaza sauti) wakati alipotembelea na kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 katika Mahafali ya 30 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza. Kushoto kwa Dkt. Kijaji na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula (Mb).
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akiangalia kipeperushi chenye maelezo ya faida za kutumia kitunguu swaumu kwa binadamu wakati Mkulima wa zao la vitunguu swaumu kutoka Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Bw, Boniface Bura, (aliyeshika kipaza sauti), akitoa maelezo namna Chuo chas Mipango ya Maendeleo Vijijini kilivyomsaidia kuongeza thamani ya zao hilo, wakati Naibu waziri huyo alipotembelea na kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa zinazotolewa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mkulima wa zao la vitunguu swaumu kutoka Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Bw. Boniface Bura, (aliyeshika kipaza sauti), alipotembelea na kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa zinazotolewa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza, kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 wa Chuo hicho wakati wa Mahafali ya 30 yaliyofanyika mara ya tano katika Kituo hicho cha Mwanza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akipokea zawadi ya Kitunguu swaumu kilichosindikwa, kwaniaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli iliyotolewa na Mkulima wa zao hilo kutoka Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Bw. Boniface Bura, anayenufaika na mradi wa kuwawezesha wakulima vijijini wa Mivaraf, ikiwa ni ishara ya kuunga mkono Jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya Viwanda.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akizungumza na vyombo vya habari baada ya kumaliza kutembelea na kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 katika Mahafali ya 30 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza.
...................................................................................................................................
Benny Mwaipaja,
WFM, Mwanza
Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amekitaka Chuo Cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini, kuhakikisha kuwa kinajielekeza kutatua changamoto zinazokwaza
maendeleo ya wananchi vijijini ili kuwafanya vijana wengi wanaokimbilia mijini
kutafuta maisha waweze kubaki kwenye vijiji vyao ambavyo vitakuwa vimepangwa
vizuri na kupatikana huduma muhimu za jamii
Dkt. Kijaji ametoa
rai hiyo mkoani Mwanza, baada ya kukagua maonesho ya bidhaa na huduma
zinazotolewa na chuo hicho katika Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa,
kilichoko eneo la Bwiru, mkoani humo.
Naibu waziri huyo
wa Fedha na Mipango amesema kuwa katika kufikia azma ya serikali ya kuwa nchi
ya viwanda ifikapo mwaka 2025, Chuo hicho kina wajibu mkubwa wa kufundisha wataalamu
watakao kuwa chachu ya kuboresha huduma na kuimarisha sekta ya kilimo ambacho
ndio nguzo kuu ya uchumi wa wananchi walio wengi vijijini.
“Ni muhimu
kuwafundisha kuwafundisha wakulima namna ya kuongeza thamani ya mazao yao,
badala ya kuuza vitunguu swaumu kilo moja shilingi 5,000, vikiongezwa thamani
tumeambiwa vitaunzwa kwa shilingi 24,000 kwa ujazo huo huo jamno ambalo ni
jema” aliongeza Dkt. Kijaji
Amesisitiza kuwa
Tanzania ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni ya viwanda ambavyo vimeanza
kuonekanana kuwataka watanzania kuwa tayari kuchukua fursa hizo, hususan vijana
mahali walipo kule vijijini badala ya kukimbilia mijini.
Kwa upande wake
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la
Ilemela, Jijini Mwanza, Bi. Angelina Mabula, amerejea wito wake kwa Halmashauri
zote nchini kutenga ardhi kwaajili ya kuendeleza vijana katika sekta ya
uzalishaji mali ili waweze kutumia uwepo wa Chuo cha Mipango katika
kuwaendeleza kwa vitendo kwa kuwapatia stadi za namna ya kujikwamua kiuchumi
Mkulima kutoka
Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, ambaye amewezeshwa na Chuo Cha Mipango kuongeza
thamani ya zao la Kitunguu Swaumu kupitia ufadhili wa Shirika la MIVARAF, Bw.
Boniface Bura, amempatia zawadi ya Kitunguu Swaumu kilichosindikwa, Rais Dkt.
John Pombe Magufuli, ikiwa ni ishara ya kuonesha furaha yake kwa mafanikio makubwa
aliyoyapata.
“Hivi sasa
ninauwezo wa kuvaa nguo mpya, nimepeleka watoto wangu shuleni na kujenga makazi
bora, hii ni fursa nzuri kwangu na wenzangu ambao kwa pamoja tumeamua kuongeza
mnyonyoro wa thamani wa zao letu la kitunguu swaumu” alisema Bw, Bura huku
akishangiliwa na watu walioshiriki kuangalia maonesho hayo
Naye Mkufunzi wa
Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Bw. Ezekiel Kanire, amesema kuwa Chuo
hicho kinafanya mawasiliano na Shirika la Viwango nchini TBS, ili iweze
kuwapatia wakulima hao wa Vitunguu wilayani Mbulu mkoani Manyara, namba ya
utambulisho ya ubora wa bidhaa ili bidhaa hizo ziweze kuuzwa pia kimataifa na
kuwaongezea wakulima hao kipato kikubwa zaidi.
Kupitia mpango huu
wa chuo wa kuwawezesha wakulima vijijini kupitia mradi wa Mivaraf, tumeweza
kuwasaidia wakulima wa vitunguu swaumu wa Mbulu mtambo wa kuchakata vitunguu
hivyo wenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 54, kinachobaki sasa ni
kuboresha zaidi uzalishaji na ufungashaji wa bidhaa hizo ili ziweze kupata namba
ya utambulisho kutoka TBS.
0 Comments