Timu za Taifa za
umri chini ya miaka 23 kwa wanaume na wanawake ambazo hazikuwa na majina sasa
zinaitwa Kilimanjaro Warriors (wanaume) wakati wanawake ni Kilimanjaro
Starlets.
Uteuzi wa majina
hayo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) katika kikao chake
kilichofanyika jana (Desemba 17, 2016) jijini Dar es Salaam.
Timu hizo ambazo
ni maalumu kwa ajili ya michuano ya Olimpiki zitaanza maandalizi yake Januari
mwakani, na wengi wa wachezaji watakaounda timu hizo zinazojiandaa kwa ajili ya
michuano ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan mwaka 2020 watatoka katika
timu za sasa za wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 (U20).
Mechi za mchujo
(qualifiers) kwa ajili ya michuano ya Olimpiki ya 2020 zitaanza mapema mwaka
2019.
..……………………………………………………………………………………..
IMETOLEWA NA
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

0 Comments