Shirika la Ndege
la Uturuki limeiongeza Zanzibar katika mtandao wa safari zake kuanzia Desemba
13, 2016. Hivi sasa shirika hilo linafanya safari 49 barani Afrika baada ya
hivi karibuni kuongeza safari ya kwenda Visiwa vya Shelisheli.
Shirika hilo
maarufu barani Ulaya kwa sasa linafanya jumla ya safari 293 duniani kote,
zikiwemo safari 50 kwenye nchi 31 za Afrika.
Likiwa ni
shirika la nne kwa kuwa na mtandao mkubwa wa safari duniani kote kuliko mashirika
mengine, Shirika la Ndege la Uturuki sasa litahudumia miji ya kimataifa 244
ikijumlishwa na Visiwa vya Zanzibar ambavyo ni maarufu kwa biashara ya viungo.
Watumiaji wa ndege za shirika hilo sasa watafurahia uzoefu watakaoupata
kutokana na safari hizo mpya zinazojumuisha miji 20 maarufu duniani kama vile Frankfurt, Muscat,
Munchen, Dubai, Paris, London, Milano, Amsterdam, Zurich, Bombay, Copenhagen,
Stockholm, Rome, Brussels, Berlin, Vienna, Hamburg, Tel-Aviv, Düsseldorf, na Prague.
Safari ya kwanza itazinduliwa
Jumanne, Desemba 13, 2016 na wasafiri wataondoka Istanbul saa 6:30 usiku na
ndege TK567 itakayowasili saa 3:30 asubuhi. Watarudi na ndege hiyo TK567 itakayoondoka
Zanzibar saa 4:25 asubuhi na kuwasili Istanbul saa 11:45 jioni.
Safari za Instanbul –
Kilimanjaro – Zanzibar – Istanbul (IST-JRO-ZNZ-IST) zitakuwa tatu kwa wiki.
Utaratibu wa kuweka mpango wa safari unapatikana
kupitia tovuti www.turkishairlines.com kama ifuatavyo::
Taarifa zaidi kuhusu ratiba ya safari:
Muda uliotajwa ni wa LMT.
Kuangalia ratiba ya safari tafadhali tazama tovuti www.turkishairlines.com, wasiliana na kituo +90 212 444 0849 au tembelea ofisi ya mauzo ya
Shirika la Ndege la Uturuki
Shirika la Ndege
la Uturuki, Inc.
Kuhusu Shirika la Ndege la Uturuki:
Lilianzishwa
1933 likiwa na ndege tano, na ni mwanachama wa Star Alliance. Kwa sasa shirika
hili lenye hadhi ya nyota nne, lina ndege 335 (za abiria na mizigo)
zinazosafiri kwenye miji 292 duniani kote na kufanya safari za ndani 243 kwenye
miji 49. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Skytrax wa 2016, Shirika la Ndege
la Uturuki lilichaguliwa "Shirika Bora la Ulaya" kwa mara ya
sita na "Shirika Bora kwa Ulaya ya Kusini kwa mara ya nane mfululizo. Baada ya
kupata tuzo mwaka 2010 ya "Shirika Bora kwa Huduma ya Chakula”, na
mwaka 2013 na 2014 kuwa "Shirika
Bora kwa Biashara ya Chakula", na "Shirika Bora kwa Biashara
ya Chakula kwa Wasafiri wa Daraja la Wafanyabiashara”, na tuzo ya "Shirika
Bora kwa Ukumbi wa Mapumziko" hapo mwaka jana, Shirika la Ndege la Uturuki lilipewa tena tuzo
ya “Shirika Bora kwa kuwa na “Ukumbi wa
Kisasa wa Chakula” na “Shirika
Bora kwa Huduma za Chakula kwa Wasafiri” kutokana na utafiti uliofanywa mwaka
huu. Taarifa zaidi kuhusu Shirika la Ndege la Uturuki zinapatikakana kwenye
tovuti yake www.turkishairlines.com au kwenye akaunti yake ya
mtandao wa kijamii wa Facebook, Twitter, YouTube, LinkedIn,
and Instagram.
Kuhusu Star Alliance:
Mtandao wa Star Alliance ulianzishwa
1997 ukiwa ni mtandao shirikishi wa mashirika ya ndege duniani ili kutoa huduma
kwa wasafiri wa kimataifa. Kukubalika kwake kwenye soko kumetambuliwa kwa tuzo
mbalimbali za Business Traveller
Magazine na Skytrax zikiwemo Tuzo ya Dunia ya Uongozi wa Soko la Usafiri wa
Anga (Air Transport World Market Leadership Award) na Shirika Bora Shirikishi
la Mashirika ya Ndege (Best Airline Alliance). Mashirika wanachama ni: Adria
Airways, Aegean Airlines, Air Canada, Air China, Air India, Air New Zealand,
ANA, Asiana Airlines, Austrian, Avianca, Avianca Brazil, Brussels Airlines,
Copa Airlines, Croatia Airlines, EGYPTAIR, Ethiopian Airlines, EVA Air, LOT
Polish Airlines, Lufthansa, Scandinavian Airlines, Shenzhen Airlines, Singapore
Airlines, South African Airways, SWISS, TAP Portugal, Turkish Airlines, THAI
and United. Kwa ujumla, mtandao wa Star Alliance sasa unasimamia zaidi safari
za kila siku 18,500 kwenye viwanja vya ndege 1,330 katika nchi 192.


0 Comments