MSHINDI
WA MASHINDANO MAALUM YA WATOTO YALIYOANDALIWA NA KLABU YA GOLF YA JWTZ YA
LUGALO HABIBA LIKULI AKIPIGA MPIRA HUKU WACHEZAJI WENZIE WAKIMUANGALIA KATIKA
HEKAHEKA ZA MASHINDANO HAYO YALIYOFANYIKA MWISHO WA WIKI JIJINI DAR ES SALAAM.
WASHIRIKI
WA MASHINDANO MAALUM YA WATOTO WAKIHAKIKI MATOKEO YAO MARA BAADA YA KUMALIZA
VIWANJA 18 AMBAPO HABIBA LIKULI ALIIBUKA
MSHINDI KATIKA MASHINDANO HAYO YALIYOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI KATIKA UWANJA WA
LUGALO JIJINI DAR ES SALAAM.
MWALIMU
WA MCHEZO WA GOLF WA KLABU YA JWTZ YA
LUGALO ELIAS CHIUNDU AKITOA
MAELEKEZO KWA WATOTO WALIOSHIRIKI MASHINDANO MAALUM YA MCHEZO HUO YALIYOFANYIKA
MWISHONI MWA WIKI JIJINI DAR ES SALAAM.
MSHINDI
WAPILI WA MASHINDANO MAALUM YA WATOTO YALIYOANDALIWA NA KLABU YA GOLF YA JWTZ
YA LUGALO SOPHIA JUMA AKIPIGA MPIRA HUKU
WACHEZAJI WENZIE WAKIMUANGALIA KATIKA HEKAHEKA ZA MASHINDANO HAYO YALIYOFANYIKA
MWISHO WA WIKI JIJINI DAR ES SALAAM.
WASHIRIKI WA MASHINDANO MAALUM YA WATOTO WAKIHAKIKI MATOKEO
YAO MARA BAADA YA KUMALIZA VIWANJA 18
AMBAPO HABIBA LIKULI ALIIBUKA MSHINDI KATIKA MASHINDANO HAYO
YALIYOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI KATIKA UWANJA WA LUGALO JIJINI DAR ES
SALAAM.
(PICHA NA Luteni Selemani Semunyu).
........................................................................................................................................
Na Luteni Selemani Semunyu
Viwango vya Watoto wanaocheza mchezo wa golf katika
klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania ya Lugalo vinazidi kupanda na kuongeza uwezekano wa kupata vipaji vipya na Wawakilishi wa Taifa.
Hayo yalisemwa na Mmoja wa Walimu wa Mchezo huo wa
Klabu ya Lugalo Elias Chiundu mara baada ya mashindano ya Watoto yaliyofanyika mwishoni
mwa Wiki katika Uwanja wa Golf wa Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waaandishi wa habari mwalimu huyo alisema
yeye kama Mwalimu anafarijika kwa kuona viwango vya watoto hao vikikua na hivyo
ni matarajio yake katika mwaka 2017 watafanya vyema Zaidi.
“Mwaka 2017 tunataraji baadhi ya watoto waliokuwa wanacheza katika Daraja la Junior
kutokana na Umri wao kuongezeka sambamba na kiwango cha uchezaji basi wataingia
katika Divisheni Nyingine na kutoa changamoto kwa waliowakuta” Alisema Chiundu.
Aliongeza kuwa kuna Faida kubwa kwa Wachezaji
kuandaliwa wangali wadogo kwani wanakuwa na kipindi kirefu cha mafanikio iwapo wataweka jitihada sambamba na
kuungwa mkono na wazazi.
Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza baada ya kucheza Viwanja 18 aliibuka Habiba Likuli baada ya kupata mikwaju ya jumla 89 kiwango chake cha
uchezaji kikiwa ni 15 na hivyo kuibuka na Mikwaju ya Jumla 72 akifuatiwa na
Sophia Juma aliyepiga Mikwaju ya Jumla 74.
Mbali na
Viwanja 18 pia katika kundi la Watoto waliocheza viwanja Tisa mshindi ni Abra Bella
aliyepiga mikwaju ya jumla 48 na katika viwanja vitatu mshindi ni Salehe Ramadhani
aliyepiga mikwaju ya jumla 17
Kwa upande wake mshindi wa mashindano hayo ya siku
moja Habiba Likuli amesema mashindano yalikuwa mazuri licha ya changamoto ya
jua kuwa kali na kuomba Wazazi kuwaruhusu watoto wao kuja kushiriki nao ili
kuonyesha vipaji na kutumia muda wao vizuri.
Jumla ya wachezaji 32 wameshiriki katika mashindano
hayo yenye lengo la kupima ukuaji wa vipaji vyao.





0 Comments