Mkurugenzi wa
Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa akizungumza na wauguzi baada ya wauguzi hao kutoa
zawadi kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo. Zawadi hizo zimepokelewa
na mtoto Neema Selemani kwa niaba ya wagonjwa wengine. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa
Jengo la watoto, NPC One, Bi. Anna
Mponeja na Katibu wa Tughe Tawi La Muhimbili, Bw. Faustine Fidelis.
Mkurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH), Bi. Agnes
Mtawa akitoa zawadi kwa mtoto Neema Selemani ambaye amepokea kwa niaba ya
wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.
Wauguzi
wakifuatilia hafla hiyo leo.
Mkuu wa Jengo la
Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja (katikati) akiwa amevishwa kitenge baada ya
kupewa zawadi na wauguzi wenzake.
Meneja kutoka majengo
mbalimbali katika hospitali hiyo wakiwa katika hafla hiyo Leo. Kutoka Kulia ni Meneja
wa Jengo la Ufuaji, Bi. Lina Kinabo, Meneja wa Jengo la Upasuaji, Bi. Jane
Chuwa, Meneja wa Jengo la Huduma za Nje, Bi. Juni Samwel na Meneja wa Jengo la
Sewahaji, Bi. Salome Mayenga.
Mkuu wa Jengo la
Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja akimkabidhi Mkurugenzi wa Uuguzi katika
hospitali hiyo, Bi. Agnes Mtawa zawadi maalamu.
Bi. Anna Mponeja
akimlisha keki mtoto Neema Seleman Leo katika hospitali hiyo.
Picha na John Stephen,
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
.......................................
Baadhi ya wauguzi wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), leo wametoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa
waliolazwa katika hospitali hiyo.
Akizungumza katika
hafla hiyo fupi, Mkurugenzi wa Uuguzi katika hospitali hiyo, Bi. Agnes Mtawa
amewashukuru wauguzi hao kwa kuonyesha ushirikiano katika kazi na kutoa huduma
nzuri kwa wagonjwa.
Mtawa aliwaasa wauguzi
kuendelea na upendo huo waliouonyesha katika kipindi chote cha mwaka 2016 kwa
kuwa ndio upendo ambao Mungu anataka wauonyeshe kwa wagonjwa.
Pia, aliwapongeza kwa kukabiliana na
changamoto mbalimbali katika mwaka huu na kuwataka kutumia changamoto hizo kama
sehemu ya mikakati ya mwaka 2017.
Naye Meneja wa Jengo la
Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja aliwashukuru wauguzi kwa kutoa huduma nzuri
kwa wagonjwa katika kipindi chote cha mwaka 2016.









0 Comments