
Waziri wa
Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametuma salamu
za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa wapiga picha pamoja na
Wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha mwanahabari na mpiga picha
Mpoki Bukuku kilichotokea leo katika Taasisi ya Mifupa (MOI)
Mhe. Nape Nnauye pamoja na
watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha
mwanahabari huyo kwani ni pigo katika tasnia ya habari nchini.
“Nimepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa ya kifo cha mwanahabari Mpoki Bukuku. Kifo chake ni pigo
katika tasnia ya habari hususani katika picha , nimehuzunishwa sana kwa
sababu Marehemu wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa kwenye vyombo
mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti ya Majira, Business Times , The
Guardian , Nipashe na Mwananchi na The Citizen.”
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina
Imetolewa na Idara ya Habari(MAELEZO)
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Dar es Salaam
23 Desemba, 2016
0 Comments