Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba wa
kulia na kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wakiangalia gari ambayo ilikamatwa Wilayani
Mkuranga Mkoa wa Pwani ikiwa na wahamiaji haramu wapatao 150 ambao ni raia kutoka nchini Ethiopia ambao walikamatwa
wakati wakiwa wapo safari kuelekea miko
ya kusini.
(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu
Nchemba kushoto akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka
wakizungumza jambo baada ya kulikagua gari ambalo lilikamatwa likiwa na wahamiaji
haramu 150 Wilayani Mkuranga Mkoa wa
Pwani ambao ni raia wa Ethiopia.
................................................................................................................................
NA VICTOR MASANGU, PWANI
KUTOKANA na kuwepo kwa ongezeko la wimbi la migogoro ya
ardhi kila kukicha katika baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Pwani kati
ya jamii ya wakulima na wafugaji na kupelekea wakati mwingine kuibuka kwa
mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yanasababisha hali ya uvunjifu wa amani
na baadhi ya viongozi na wananchi wengine kupoteza maisha kikatili kimeundwa kikosi kazi maalumu kwa
ajili ya kuweza kukomesha kabisa vitendo
hivyo.
Matukio ya namna hiyo katika
Mkoa wa Pwani yanaonekana kumsikitisha
na kumlazimu Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba kuingilia kati sakata
hilo kwa kutangaza rasmi kupambana vilivyo na watu wote ambao watabainika wanajihusisha
na vitendo hivyo vya mauaji ili waweze kukamatwa haraka na kuweza kufikishwa katika vyombo vya dola
ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Waziri
nchemba ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kuwatembelea
askari polisi, magereza, uhamiaji pamoja zimamoto wa Mkoani Pwani kwa
ajili ya
kuweza kukagua shuguli mbali mbali za
utekelezaji ya majukumu yao ya kila siku ikiwemo na kuweza kubaini
changamoto zinazowakabili pamoja na kuweka mikakati kwa ajili ya
kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
“Kumekuwepo
katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani kuna baadhi ya viongozi wa vijiji
pamoja na wakulima na wafugaji kupoteza maisha, kwa hili sisi kama Wizara
hatuwezi kulivumilia hata kidogo kwani kwa sasa tumejipanga ii kuweza kuwabaini
watu ambao wanahusika katika vitendo hivyo,”alisema Waziri.
Alisema kuwa anasikitishwa kuona mauaji yanafanyika kitu
ambacho ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi, kwa mwananchi yoyote
kuamua kujichukulia sheria mikononi kwa kufanya vitendo vya mauaji hivyo
ameahidi kulivalia njuga suala hilo na wale wote watakaobainika wataweza
kuchukuiwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama
hiyo.
Aidha Waziri Nchemba alibainisha kuwa kutokana na kuwepo kwa wahamiaji haramu ambao wanaingia nchini
bila ya kuwa na vibali Wizara yake imeweka mikakati kabambe ya kuongeza doria
usiku na mchana katika sehemu mbali
mbali ikiwemo mipaka, fukwe za bahari
pamoja na bandari bubu amabzo zimekuwa zikitumika kuwapitisha raia hao wa
kigeni.
“Tatizo lawahamiaji haramu katika Mkoa wa Pwani bado ni
tatizo kubwa kwani imekuwa ndio kama lango la kuingilia pindi wanapokuja hasa katika maeneo ya Wilaya ya Bagamoyo
pamoja na Wilaya ya Kibaha, hivyo sisi katika hili tumeshajipanga ili kuweza
kuthibiti njia zote ambazo wamekuwa wakizitumia katika kupita,”alisema Nchemba.
Pia katika hatua nyingine Nchemba alitoa wito kwa wananchi
wote kushirikiana bega kwa began a serikali pamoja na vyombo vya dola katika
kuwabaini na kuwafichua watu ambao
wanakuwa na mashaka nao kwani wengine wanaingia nchini kwa ajili ya kufanya
matukio mbali mbali ya uharifu wa kutumia siraha.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry
Koka ameiomba serikali ya awamu ya tano kupitia
Wizara ya mambo ya ndani kuhakikisha inaongeza vitendea kazi pamoja na
kuongeza ujenzi wa vituo vingine vidogo vya polisi ambavyo vitaweza kusaidia kuimarisha hali ya ulinzi na usalama pamoja na
kupamba na waharifu ambao wanaingia Mkoa wa Pwani kinyemela na kujificha.
Pia Koka alimwomba waziri wa mambo ya ndani kuweka utaratibu
wa kuhakikisha vituo vidogo vya polisi vilivyojengwa vinakuwa wazi wakati wote
lengo ikiwa ni kuweza kupambana na matukio mbali mbali ya uharifu ambayo
yanakuwa yanajitokeza bila ya kuwa na muda maalumu hivyo vituo vikiwa wazi kutaweza
kusaidia kupunguza hali ya uharifu.
MATUKIO ya vitendo vya mauaji katika baadhi ya maeneo Mkoani Pwani ambayo yanawahusisha wakulima na wafugaji
pamoja na baadhi ya viongozi wengine bado
yanaonekana kuwa ni tishio na kuendelea kufanyika hivyo kunahitajika jitihada
za makusudi zifanyike kutoka serikalini
ili kuweza kutatua migogoro hiyo na kurudisha hali ya amani na utulivu kwa wananchi.


0 Comments