Meneja
wa kanda ya kaskazini wa Benki ya KCB Tanzania Judith Lubuva, akiongea na wanawake wajasiriamali
waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani Arusha.
Afisa Mawasiliano ya Umma wa benki ya KCB
Margaret Makere akiongea na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya
ujasiriamali yaliyotolewa na benki hiyo mkoani Arusha.
Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji
na Ushindani Tanzania (TECC) Nina Nchimbi akitoa mafunzo ya ujasiriamali
yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa
Arusha.
Meneja
wa kanda ya kaskazini wa Benki ya KCB Tanzania Judith Lubuva (aliyekaa wapili kulia) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali waliohudhuria na kumaliza
mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na benki hiyo katika mkoa wa Arusha.
...................................................................................
Katika swala
zima la kumkomboa mwanamke mjasajiriamali, Benki ya KCB Tanzania inaendelea na
programu ya mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali yanayoitwa 2JIAJIRI. Programu
hii inalenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika changamoto
zinazosababisha biashara yake ishindwe kuendelea.
Benki ya KCB
imepanga kufundisha wanawake wajasiriamali 315 kutoka mikoa ya Dar Es salaam,
Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na Zanzibar ambapo matawi ya benki hiyo
yapo.
Mafunzo haya ni
bure kabisa, benki ya KCB inagharimia gharama zote. na yanahusisha Elimu
ya Fedha (Financial Literacy), Kufikiwa huduma za kifedha (Financial
Inclusion), Masuala ya Kisheria (Legal Framework), Ushindani wa Kibiashara (Business
Competitiveness) na kuwa na sifa za kukopesheka (How to be bankable).
Zaidi ya mafunzo
hayo, benki ya KCB itawapatia wanawake wajasiriamali hao maafisa watakao
wafundisha kwa vitendo kwenye maeneo ya biashara zao. Maafisa hao watakua ni
afisa fedha, afisa sharia na afisa masoko.
Kwako mwanamke
mjasiliamali “JIULIZE KWANINI uhangaike
wakati benki ya KCB tupo!”




0 Comments