Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata
utepe kuzindua rasmi Makao Makuu ya Wizara yaliyopo katika jengo la
Masomo ya Biashara na Sheria katika Chuo Kikuu cha Dodoma ambako Wizara
imehamia rasmi makao maku ya Serikali mkoani Dodoma
Katibu Mkuu Prof sifuni Mchome akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Waziri Dkt
Mwakyembe mara baada ya kukata utepe na kuzindua rasmi ofisi za wizara
mjini Dodoma
Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya
kukata utepe na kuingia ndani ya jengo la Wizara ambako alizindua rasmi
ofisi za wizara mjini Dodoma
Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe katika picha ya pamoja na watumishi na
wageni wake mara baada ya kuzindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma ambako wizara imehamia rasmi mkoani Dodoma
Waziri wa Mambo ya Katiba na
Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua rasmi Ofisi za wizara yake mkoani
Dodoma na kuwataka Watumishi wa wizara waliohamia Makao Makuu ya Serikali, Dodoma
kutekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa.
Dkt Mwakyembe amezindua
rasmi makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria yaliopo mkoani Dodoma katika
viunga vya Chuo Kikuu cha Dodoma baada ya wizara hiyo na
watumishi wake 31 kuhamia rasmi makao makuu ya Serikali mkoani Dodoma.
Baada ya uzinduzi huo Mhe.
Mwakyembe alisema kitendo cha kuhamia mkoani DODOMA ni utekelezaji wa agizo la
kuhamia makao makuu ya Serikali ambalo lilitolewa mwezi Julai mwaka 2016 na
hivyo watumishi wanapaswa kutekeleza majukumu yao na kuwahudumia wananchi kama
walivyokuwa Dar es salaam.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na
Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, Mkuu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kanda
ya Dodoma, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma, Prof Kikula na watumishi 31 wa wizara
ambao wamehamia Dodoma katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa agizo hilo la
Serikali.
Awamu ya Kwanza yenye
watumishi 31 wa wizara wakiongozwa na Waziri Dkt Dkt. Harrison Mwakyembe,
Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju imehamia rasmi
mkoani Dodoma. Awamu ya pili na ya tatu zitafuata utaratibu ambao umewekwa na zoezi
hilo linatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2018.
Kufuatia kuhama rasmi kwa
ofisi za wizara sasa mawasiliano yote yatafanywa kupitia anuani ya Katibu Mkuu Sanduku
la Posta 315 Dodoma, namba ya simu ni 026 2321680, nukushi ni 026 2321679 na
baru pepe ni ile ile ya km@sheria.go.tz







0 Comments