Na: Frank Shija – MAELEZO
Mwili wa aliyekuwa Mgombea wa
kwanza Mwanamke kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Anna Senkoro unatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi tarehe 07/01/2017
kuanzia saa 8:00 mchana.
Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Bwana. Fred Sendim ambaye ni Msemaji wa Familia ya marehemu Dkt. Senkoro.
“Mipango ya mazishi inaendelea
vizuri nyumbani kwake Segerea, pia nitumia fursa hii kutoa shukrani za
kipekee kwa wote wanaoendelea kutufariji na kushirikiana nasi bega kwa
bega katika kipindi hiki kigumu.” Alisema Sendim.
Msemaji huyo wa familia amesema
kuwa taratibu za mazishi zitataunguliwa na Ibada maalum itakayoambatana
na utoaji wa heshima za mwisho kuanzia saa Saba mchana katika Kanisa la
Winners lililopo Banana, Ukonga jirani na Kituo cha Mafuta cha Oil
Com.
Awali akielezea kifo chake
msemaji wa familia hiyo amesema kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na
ugonjwa wa moyo ambapo juzi tarehe 04 majira ya saa 11 alfajiri
alizidiwa na kupelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu katika Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na baadaye alihamishiwa Hospitali ya
Taifa Muhimbili ambapo alifikwa na mauti mnamo saa 3:30 asubuhi.
Dr.Anna Senkoro alikuwa mgombea
wa kwanza mwanamke kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania mwaka 2005 kupitia Chama cha APPT Maendeleo, Marehemu ameacha
watoto wa tatu na wajukuu wa wiwili.
Mungu hailaze roho ya Maerehemu mahali pema peponi amina.

0 Comments