Mwenyekti wa Klabu ya Golf ya Jeshi ya Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo akizungumza na Wachezaji wa Klabu hiyo Jijini
Dar es Salaam,wachezaji hao wanataraji Kuwakilisha katika mashindano ya Miaka
10 ya Klabu yanayotarajiwa kufanyika Mwezi February mwaka huu.
(Picha na Luteni
Selemani Semunyu).
Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania ya Lugalo Brigedia jenerali Michael Luwongo akisisitiza jambo
wakati akizungumza na Baadhi ya Watendaji wa klabu hiyo hawapo pichani kuhusu maandalizi ya Miaka 10 ya Klabu hiyo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wachezaji wa kulipwa na wale wa Ridhaa wa Klabu ya Golf ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wakiwa katika mazoezi kwa Ajili ya Maandalizi ya mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu hiyo yanayotarajiwa kufanyika Mwezi February Mwaka huu 2017 Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Luteni Selemani Semunyu) .
Baadhi ya Wachezaji wa kulipwa na wale wa Ridhaa wa Klabu ya
Golf ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wakijadiliana wakati
wa mazoezi kwa ajili ya mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu hiyo
yanayotarajiwa kufanyika Mwezi February
Mwaka huu 2017 Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Luteni Selemani Semunyu)
........................................................................................
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ.
Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya
Lugalo iko katika maandalizi ya viwanja kwa ajili ya mashindano ya kuadhimisha
miaka 10 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 2006.
Akizungumza na waandishi wa Habari msimamizi wa
viwanja ambaye pia ni mchezaji wa kulipwa wa klabu ya Lugalo David Helela alisema
kila kitu kinaenda sawa na wanaangalia sehemu ngumu kuchezeka kuondoa vikwazo
visivyo na sababu.
“kuna vikwazo vinavyopaswa kuwepo katika Uwanja wa
golf lakini kuna vikwazo vingine vinakuwepo
lakini havina sababu wala havina mchango katika kuonyesha umahiri wa mchezaji
hivyo tunaviondoa”, Alisema Helela.
Aliongeza kuwa mbali na kuviondoa bado viwanja kama
namba 12 vitaendel;ea kuwa moja ya kiwanja kigumu kwa mchezaji atakayecheza
katika uwanja huo kutoka na jinsi ulivyowekwa kwa lengo tu la kukamilisha sifa
za uwanja wa Golf.
Helela Alisema katika kuelekea kuadhimiasha Miaka 10
klabu ya lugalo itabaki kuwa ndio klabu pekee inayothamini kwa kiwango kikubwa
mchango wa wachezaji wa kulipwa ambao mbali na kuwatumia katika kufundisha
vijana na kusimamia sheria za mchezo
lakini wamekuwa wakishirikishwa katika mashindano ya wachezaji wa
kulipwa .
Kwa Upande wake Afisa Tawala wa Klabu hiyo Kapteni
Amanzi Mandengule alisema amefanya ukaguzi wa Awali kazi zinaenda vizuri na
kutoa wito kwa wadhamini kuongeza nguvu ili kuwa na mashindano Bora.
“ Kuna wadhamini tuliofanikia na wako tayari na
wameanza maandalizi lakini Milango iko wazi kwa wadhamini wengine kujitokeza
kwani Mashindano ya Miaka 10 ya Klabu yanatarajiwa kuwa ya Aina yake
ukilinganisha na mashindano yaliyowahi kuandaliwa”Alisema kapteni Mandengule.
Aliongeza kuwa taarifa rasmi ya mashindano na Mgeni
rasmi inatarajiwa kutolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Klabu Brigedia
Jenerali Michael Luwongo ili kuelezea kwa kina mashindano hayo yanayotarajiwa
kufanyika katikati ya Mwezi wa Pili.
Katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa ya siku
tatu Vilabu vyote vimealikwa na makundi yote ya mashindano yatashirikishwa
katika mashindano hayo ambayo yatakuwa ni mashindano ya Kwanza makubwa nchini kwa
mwaka 2017 .




0 Comments