Mwenyekiti wa Kitengo cha Nafaka na Mamalishe wa
Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam,Bw.
Mohamed Salum akielezea jambo kwa mwandishi wa habari kuhusu hali ya
upatikanaji wa chakula katika Soko hilo leo jijini Dar es Salaam. Mohamed
amesema kuwa chakula kinapatikana kwa wingi kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa.
Picha ikionyesha baadhi ya nafaka zikiwa
zinauzwa katika Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mkazi wa jijini Dar
es Salaam akinunua nafaka katika Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Picha na: Frank Shija
– MAELEZO.
......................................................................................
Na: Frank Shija –
MAELEZO.
HALI ya upatikanaji
wa chakula nchini inaridhisha licha ya changamoto ya kuongezeka kwa bei ya bidhaa
za chakula zitokanazo na nafaka.
Hayo yamebainishwa na
Mwenyekiti wa Kitengo cha Nafaka na Mamalishe wa Soko la Kisutu jijini Dar es
Salaam, Bwana Mohamed Salum katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii
leo jijini Dar es Salaam.
Mohamed amesema kuwa
pamoja na kuwa Dar es Salaam inategemea chakula kutoka mikoani bado hali ya
upatikanaji wake ni mkubwa na wa kuridhisha kama ambavyo imekuwa miaka ya
nyuma.
“Chakula bado
kinapatika kwa wingi japo changamoto iliyopo ni ongezeko la bei pekee kitu
ambacho si kigeni duniani kote,” alisema Salum.
Alisema nia ajabu
sana kusikia watu wanasema kuna baa la njaa wakati vyakula vinapatikana kwa
wingi katika masoko yetu.
Aliongeza kuwa
kungekuwa na tatizo la uhaba wa chakula basi hata uingizwaji wa chakula katika
jiji la Dar es Salaam ungepungua kwani asilimia kubwa inategemea chakula kutoka
mikoani, badala yake upatikanaji wa chakula umeendelea kuwa wa kuridhisha.
“Ndugu mwandishi
ukitaka kujua kuwa hakuna uhaba wa chakula jaribu kutembelea maeneo ya Manzese
Uzuri utajionea namna maroli matani kwa matani yanayoingiza nafaka kwenye mashine
za kusaga na kukoboa.” Alisisitiza.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment