JAFO AONYA UVUVI HARAMU WILAYANI MAFIA - MTAZAMO MEDIA

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 15 January 2017

JAFO AONYA UVUVI HARAMU WILAYANI MAFIA

Na Mwamvua Mwinyi,Mafia
..................................

NAIBU Waziri Tamisemi ,Selemani Jafo amemtaka afisa Uvuvi wa halmashauri ya wilaya ya Mafia,mkoani Pwani kuhakikisha anadhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu na kama uvuvi huo utaendelezwa afisa huyo atawajibishwa.

Sambamba na hayo ameeleza halmashauri ya wilaya ya Mafia hali sio shwari hivyo watendaji wajitume kwa kufuata kasi ya serikali iliyopo madarakani.

Alisema, matumizi ya mabomu yamekua mwiba kwa mazalia ya samaki baharini ambayo madhara yake ni makubwa kwa nyakati zijazo ambayo yanatakiwa kudhibitiwa mapema.

"Nikisikia uvuvi haramu wa kutumia mabomu unaendelea huku samaki wakifa na kupunguza ongezeko, afisa uvuvi kazi hana, kwasababu tunaendelea kutoa maagizo lakini hakuna usimamizi mzuri"alisema Jafo.

Alisema, uvuvi haramu matumizi ya mlipuko na nyavu hazistahili kutumika katika kuvua samaki na ni jambo la hatari.

Aliwataka watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea  kwani baadhi ya mambo yanaendelea kuzorota kwa kutokua na mabadiliko.

Jafo alisema, athari kubwa itakua kwa kwa watu ambao watashindwa kufuata maelekezo ya viongozi.

Aidha alisema Halmashauri ya wilaya ya Mafia bado hali si nzuri kutokana na utendaji mbovu na kama wapo watendaji wataendelea kutowajibika na kubadilika hatua zitachukulia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages