Mwanasheria na msemaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya RZ Frances Kiganga ,akielezea chanzo cha mgodi huo kujifunika.
IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE
WATU
kumi na nne(14)mmoja akiwa ni Raia wa China wamefukiwa na udongo usiku
wa kuamkia leo majira ya saa saba usiku (7:00)wakiwa wanaendelea na
majukumu yao ya uchimbaji kwenye kampuni ya RZ Iliyopo kijiji cha
Nyarugusu wilayani na Mkoa wa Geita.
Sababu
za kuporomoka udongo ni kutokana na mgodi kuchimbwa zamani na
Wajerumani hivyo kupelekea baadhi ya maeneo hayo kuwa na nyufa na vyuma
kushindwa kushikilia udongo wa juu hali ambayo imepelekea kuzidiwa na
mwisho wa siku kuporomoka.
Kamati
ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita,ikiongwaza na mkuu wa Mkoa huo
Meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga imefika katika Mgodi wa RZ
kuangalia na kujionea zoezi la ukoaji .
Kamisha
msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria Mhandisi Yahaya Samamba
,ameelezea kuwa jitihada ambazo zimefanyika ni kuwasiliana na migodi
iliyopo karibu na eneo hilo na pia wameshaomba msaada Kahama na kwenye
mgodi wa GGM kupatiwa vifaa vya uokoaji ili zoezi hilo liwezekufanikiwa
kwa urais zaidi.
“Jitihada
ambazo tumezifanya hadi sasa tumeomba msaada kahama na kwenye mgodi wa
Geita,kupatiwa vifaa ambavyo vitasaidia kwa wepesi zoezi hili la uokoaji
ingawa tumeshapata vifaa vingine kutoka kwenye mgodi wa Busolwa”Alisema
Samamba.
Kamanda
wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Geita.Elisha Mugisha,amesema
kuwa eneo la chini ambalo limefukiwa na udongo ndio ambalo kwa sasa
wanaendelea kulitanua ili sehemu hiyo iwe kubwa watu waweze kupita.
“Eneo
lote lile la chini limefukiwa na udongo lakini kule chini kunaonekana
kuna sehemu za kwenda pembeni ingawa limefukiwa lakini chini
kunauhimala kunauwezekano kule chini wale watu wapo hai na
wamepelekewamipira ya hewa na kazi inayofanyika ni kutanua eneo ambalo
litasaidia kuwatoa watu hao”tumekwisha kupeleka mipira
Mwanasheria
na msemaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya RZ Frances Kiganga
ameelezea kuwa chanzo kikubwa ni mashimo ya zamani kwani udongo
unapotikisika umekuwa ukisababisha baadhi ya nyufa kuendelea kupata
shida.
Baadhi
ya wafanyakazi wa kampuni hiyo Charles Julius Na Robert Stanleyambao
wameeleza kuwa mida ya saa saba usiku duara lilinza kushuka taratibu na
baada ya hatari hiyo walipewa taarifa ya watu ambao walikuwa chini
kupandisha juu lakini hata hivyo jitihada hizo hazikuzaa matunda.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amewataka wanaosimamia zoezi la uokoaji kuongeza nguvu ya uokozi .
Hadi
Madukaonline inaondoka kwenye eneo la tukio akuna mtu yoyote ambaye
ameokolewa ingawa jitihada bado zinaendelea kwa kuomba mashirika kuweka
msaada zaidi wa uokoaji.
|
0 Comments