Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akizindua kitabu cha Mwongozo
wa Taifa wa Utekelezaji wa Sera za Huduma kwa watoto waliokatika mazingira
hatarishi kwa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio
kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Misaada na Maendeleo la
Marekani (USAID) nchini Tanzania Tim
Donnay, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Naibu Katibu
Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Dkt.
Zainab Chaula na Msaidizi wa Waziri wa Nchi TAMISEMI Bi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia
Mmbando akimkabidhi Mkurugenzi wa Jiji
la Dar es Salaam kitabu cha Mwongozo wa Taifa wa Utekelezaji wa
Sera za Huduma kwa Watoto waliokatika mazingira hatarishi kwa Serikali za Mitaa
leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene na Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI
Dkt. Zainab Chaula (wapili kulia).
Baadhi ya washiriki wa mkutano baina ya USAID na
TAMISEMI uliofanyika katika ofisi za TAMISEMI jijini Dar es Salaam wakifuatilia
hoja kutoka kwa wasilishaji wa mada leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Andrew Komba
akichangia mada wakati wa mkutano baina ya TAMISEMI na USAID kuhusu Afya ya
mama na motto leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akiteta jambo na Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID) nchini
Tanzania Tim Donnay mara baada ya kumaliza mkutano kuhusu Afya ya Mama na Mtoto
leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja
washiriki wa mkutano baina ya TAMISEMI
na USAID kuhusu Afya ya mama na mtoto leo jijini Dar es Salaam.Kutoka Kulia ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Mpoki, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID) nchini Tanzania Tim Donnay, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
.................................................................
Na:
Frank Shija – MAELEZO
26/01/2017
WAKUU wa Mikoa na
Wilaya nchini wametakiwa kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Agizo hilo limetolewa
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) George Simbachawene wakati akizungumza na wanaandshi wa habari baada
ya kumaliza mkutano wa pili wa majadiliano baina ya TAMISEMI na Shirika la
Maendeleo la Marekani (USAID) pamoja na uzinduzi wa Muongozo wa Taifa wa
Utekelezaji wa Sera za Huduma kwa watoto waliokatika mazingira hatarishi leo
jijini Dar es Salaam.
“Sera
ya ugatuaji wa madaraka inaipa mamlaka Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha watoto wanaishi katika mazingira
salama, natoa wito kwa Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya nchini kutimiza wajibu wao
kwa kushugulikia changamoto za watoto wa mitaani,” alisema Simbachawene.
Simbachawene aliongeza
kuwa Serikali za Mitaa zinao wajibu wa kuwahudumia watoto wanaoishi katika
mazingira magumu kwa ndiyo watekelezaji wa sera mbalimbali ikiwemo sera ya
watoto, viongozi wa Serikali za Mitaa wasiishie tu kuwaondoa watoto mitaani
bila ya kutafuta kiini na suluhisho la tatizo hilo.
Aidha Simbachawene
amempongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kwa kazi nzuri ya utafiti ambayo imebaini kuwa rasilimali nyingi zinazotengwa
kwa ajili ya kuhudumia afya ya mama na motto haziwafikii walengwa ambapo
amesema kuwa hiyo ni changamoto kubwa.
Aliongeza kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli inasisitiza uwazi na
uwajibikaji hivyo panapotea kuwa uzembe unatokana na utendaji mbovu miongoni
mwetu si vyema tukafumbia macho badala yake inapaswa tuseme ukweli ili wahusika
wajirekebishe na kuchukuliwa hatua stahiki.






0 Comments