Jitihada
mbalimbali zinafanywa ili kuhakikisha TRA inaongeza makusanyo kwa kuongeza
ufanisi katika ukusanyaji, kuhimiza maadili mema kwa watumishi, kuboresha
mifumo ya ukusanyaji, kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wananchi
katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kufuatili, kuhimiza
matumizi ya mashine za kielektronik na kuhimiza ulipaji wa kodi ya majengo.
TRA
inaendelea kuhimiza wafanyabiashara wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) kuwasilisha ritani za VAT kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi kama
ilivyobadilishwa katika Sheria ya Fedha ya 2016.
Pamoja
na hayo tunawakumbusha na kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam ambao
hawajafanya uhakiki wa taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN)
kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe 31 Januari 2017 ili zoezi hilo liweze
kuanzishwa katika mikoa mingine.
TRA
inatoa wito kwa wafanyabiashara kulipa kodi stahiki kwa hiari na wakati ili serikali
ipate mapato yake ambayo yataiwezesha kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.
Kwa
wafanyabiashara wenye madeni ya nyuma wanashauriwa kujitokeza kuonana na
Mameneja wa Mikoa na Wilaya kujadiliana jinsi watakavyolipa madeni yao bila
kuathiri biashara zao.
Wamiliki
wa majengo wanaaswa kutoa ushirikiano kwa kulipia ankara zao za kodi ya majengo
kwa hiari .
‘Pamoja
Tunajenga Taifa Letu’
Richard
M. Kayombo
MKURUGENZI
WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
No comments:
Post a Comment