Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva wa
pili kulia wakiongoza mazoezi wakati wa uzinduzi wa mazoezi katika mkoa huo
uliofanyika wilaya ya Temeke yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva
anayemfuatia kulia wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanamazoezi
wakati wa uzinduzi wa mazoezi mkoa huo katika wilaya ya Temeke yaliyofanyika
leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva kushoto akiongea
na wanamazoezi wa mkoa wa Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mazoezi mkoa huo
katika wilaya ya Temeke yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam kulia ni Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
NA
Ally Daud-WIZARA YA AFYA.
MASHINDANO ya vikundi vya kufanya mazoezi
yanatarajiwa kuanza hivi karibuni jijini Dar es salaam na mikoa mingine ili
kutekeleza kauli na agizo la Mhe. Makamu wa Rais wa Awamu ya Tano Bi. Samia
Suluhu Hassan alilolitoa wakati anazindua kampeni ya kitaifa ya kufanya maoezi
Desemba 17 2016.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
jamii, jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mazoezi
ya hiari mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika katika wilaya ya Temeke.
“Hata kama zawadi ikiwa ng’ombe lazima kipatiane
kikundi kimoja cha mazoezi ambacho ni bora kuliko vikundi vingine mkoa mpaka
kitaifa ili kuwafanya watanzania waepuke magonjwa yasioambukiza kwa kupenda
mazoezi.
Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa kampeni hiyo ya
kufanya mazoezi inalenga zaidi kupunguza gharama za kutibu ugonjwa huo na
badala yake kuwataka watazania kufany mazoezi siku tatu katika wiki ngalau kwa
dakika 30 il kujikinga na magonjwa yasiomabukiza.
Kwa upande wake Mkuu Wa wilaya ya Temeke Bw. Felix
Lyaniva amesema kuwa mazoezi hayo yamewahamasisha na wamepanga kila ijumaa
wafanyakazi wote wa umma wanatakiwa kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa
yasioambukiza.
Aidha Bw. Lyaniva amesema kuwa wtanzania wanapaswa
kufanya mazoezi ili kuweza kujipunguzia gharama za matibabu ya magonjwa
yasioambukiza ili kujenga taifa lenye wananchi wenye afya imara.
Kampeni hiyo ya kufanya mazoezi ya kitaifa ina lengo la kujikinginga na magonjwa
yasioambukiza kam vile kisukari, magonjwa ya moyo, saratani, shinikizo la damu
na magonjwa ya mfumo wa hewa.
No comments:
Post a Comment