Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani akiwasalimia wachezaji wa Karakana City
wakati akikagua timu za mchezo wa Nage zilizoingia Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017. Aliyevaa
kofia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ambaye ndiyo mwandaaji wa Mashindano hayo. Ngonyani
aliyafunga Mashindano hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja,
Zanzibar. Katika mashindano hayo, timu ya Six
Centre iliibuka mshindi dhidi ya timu ya Karakana City zote za mjini Unguja.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Edwin Ngonyani akizungumza na mamia ya wananchi waliouhudhuria katika
Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP katika Uwanja wa Amani, mjini
Unguja, Zanzibar. Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ambaye ndiyo mwandaaji wa
Mashindano hayo. Ngonyani aliyafunga Mashindano hayo yaliyofanyika katika
Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala. Katika
mashindano hayo, timu ya Six Centre iliibuka mshindi dhidi ya timu ya Karakana
City zote za mjini Unguja.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza kabla ya
kumkaribisha Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Edwin Ngonyani (wapili kulia) kuja kufunga Fainali ya Mashindano ya
Nage Mapinduzi CUP 2016-2017 katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Katika
hotuba yake Masauni ambaye ndiyo aliyeandaa msahindano hayo alisema, mchezo huo
utazidi kuthaminiwa ili kuwaweka vijana pamoja.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, (aliyevaa koti) akilikabidhi Kombe la Ushindi wa Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017 kwa wachezaji wa timu ya Six Centre ya Mwera ambao waliibuka kidedea dhidi ya timu ya Karakana City. Mashindano hayo yalifanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Wapili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye ndio mwandaaji wa Mashindano hayo. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala
Msanii wa kizazi kipya, Kheri Sameer Rajab (Mr.
Blue), akitoa burudani huku akishangiliwa na Waheshimiwa Wabunge pamoja na
Wawakilishi wakati wa Fainali za Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017
yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. , Watatu kushoto
ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akifuatiwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa katika picha ya
pozi na Msanii wa nyimbo za Singeli, Manfongo kabla ya msanii huyo kupanda
jukwaa kutoa burudani katika Fainali za Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP
2016-2017, yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja Zanzibar. Wasanii
mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Visiwani walitoa burudani katika fainali
hiyo ambapo timu ya Six Centre iliibuka kidedea dhidi ya Karakana City, zote za
mjini Unguja. Mashindano hayo yaliandaliwa na Mhandisi Masauni ili kukuza
vipaji vya vijana.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa katika picha ya
pozi na Msanii wa nyimbo za Singeli, Manfongo kabla ya msanii huyo kupanda
jukwaa kutoa burudani katika Fainali za Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP
2016-2017, yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja Zanzibar. Wasanii
mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Visiwani walitoa burudani katika fainali
hiyo ambapo timu ya Six Centre iliibuka kidedea dhidi ya Karakana City, zote za
mjini Unguja. Mashindano hayo yaliandaliwa na Mhandisi Masauni ili kukuza
vipaji vya vijana.
Picha zote na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment