Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akisalimiana na
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje baada ya kuwasili
wilayani Mpwapwa kutembelea kata ya Ngh’ambi inayotarajia kufanya uchaguzi
mdogo Januari 22 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akisalimiana na Mkuu
wa Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe baada ya kuwasili wilayani Mpwapwa
kutembelea kata ya Ngh’ambi inayotarajia kufanya uchaguzi mdogo Januari 22
mwaka huu.Katikati ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje.
Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) akiongoza kikao cha kupokea taarifa kuhusu
mwenendo wa uchaguzi mdogo wa Kata ya Ngh’ambi unaotarajiwa kufanyika Januari
22 mwaka huu.Kulia kwake ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed
Maje, Mkuu wa Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe na kushoto kwake
ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa
NEC Bw. Emmanuel Kawishe, Mkuu wa Kanda ya Kati ya Uchaguzi Bi. Saada Kangeta
na Afisa Utumishi wa Tume Athumani Masesa.
Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa
Jabir Shekimweri wakati alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kutembelea Kata
ya Ngh’ambi.Kulia ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje.
Msimamizi wa Uchaguzi
Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje (aliyesimama) akitoa maelezo ya kumkaribisha
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia
kwake) baada ya kuwasili kwenye Kata ya Ngh’ambi kufuatilia mwenendo wa
uchaguzi mdogo wa diwani wa kata hiyo unaotarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka
huu.
Msimamizi Msaidizi wa
Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (wa pili kulia) akimueleza Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (wa pili kushoto
aliyekaa) kuhusu mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa Kata hiyo unaotarajiwa kufanyika
tarehe 22 Januari mwaka huu.Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC
Bw. Emmanuel Kawishe, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje
(katikati) na kulia ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo Clemence
Fugusa.
Msimamizi Msaidizi wa
Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (aliyesimama) akitoa taarifa ya mwenendo
wa Uchaguzi Mdogo wa kata hiyo.
Mkurugenzi wa Huduma
za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe (kushoto)
akifafanua jambo kwenye kikao cha kupokea taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mdogo
wa Kata ya Ngh’ambi unaotarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka huu.
Msimamizi wa Uchaguzi
Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) na Mkurugenzi wa
Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.Emmanuel Kawishe
baada ya kikao cha kupokea taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa Kata ya
Ngh’ambi.
Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akikagua daftari la
kudumu la wapiga kura kwenye kituo cha kupigia kura cha Kata ya Ngh’ambi
kilichopo kwenye Zahanati ya Ngh’ambi. Kushoto kwake aliyevaa miwani ni Afisa Uchaguzi halmashauri ya wilaya ya
Mpwapwa Bi. Martina Batholomeu.
Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (aliyevaa kofia nyeusi) akipokea maelezo kuhusu mabango ya Uchaguzi
kutoka kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (wa
tatu kushoto) wakati alipokuwa akikagua mabango hayo nje ya kituo cha kupigia
kura cha Kata ya Ngh’ambi kilichopo kwenye Zahanati ya Ngh’ambi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R)
Semistocles Kaijage (kulia) akieleza jambo baada ya kukagua mabango ya Uchaguzi
kwenye kituo cha kupigia kura cha kata ya Ngh’ambi.Katikati ni Mkurugenzi wa
Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe na kushoto ni Afisa Uchaguzi halmashauri ya wilaya ya
Mpwapwa Bi. Martina Batholomeu.
Picha
na Hussein Makame, NEC
.........................................................................
Hussein Makame, NEC-Mpwapwa
Mwenyekiti wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage amesema kila kitu kiko
sawa tayari kwa uchaguzi mdogo wa kumpata diwani wa kata ya Ngh’ambi iliyoko katika
halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mhe. Jaji (R) Kaijage ameyasema hayo
kutokana na kuridhishwa na maandalizi ya uchaguzi mdogo wa kata ya Ngah’ambi
baada ya kutembelea na kufuatilia mwenendo wa uchaguzi wa kata hiyo unaotarajiwa
kufanyika tarehe 22 Januari mwaka huu.
Akitoa taarifa fupi ya mwenendo wa
uchaguzi mdogo wa kata hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje alisema karibu vifaa vyote
kwa ajili ya uchaguzi huo vimepokelewa na kampeni za uchaguzi huo zinaendelea kwa
amani na utulivu.
Alisema baada ya uteuzi wa wagombea
kufanyika Desemba 22 mwaka 2016 wagombea wanne kutoka vyama vya ADC, CCM,
CHADEMA na CUF waliteuliwa ambao ni David Mazengo, Richard Kaleme, Leornard
Majenda na Hassan Kiuka, mtawalia.
Kwa upande wa pingamizi kwa wagombea,
Bw. Maje alisema walipokea pingamizi kutoka vyama vya CHADEMA na CCM ambapo
mgombea wa CHADEMA alipinga uteuzi wa mgombea wa CCM kwa madai kuwa si mkazi wa
halmashauri husika.
“Pingamizi hili lilitolewa uamuzi na
wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa kutupilia mbali madai hayo
baada ya uthibitisho kuwa mgombea wa CCM
ni mkazi halali wa halmashauri husika.Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo pia
alikubaliana na uamuzi wa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata.” alisema
Bw. Maje na kuongeza kuwa:
“Mgombea wa chama cha CCM alipinga
uteuzi wa mgombea wa chama cha CHADEMA kuwa fomu ya uteuzi namba 8 C sehemu C
na D imesainiwa na mtu ambaye si Katibu wa chama husika wa mkoa au Wilaya”
“Pingamizi hili pia lilitolewa uamuzi
na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa kutupilia mbali madai
hayo baada ya uthibitisho wa maandishi kuwa aliyesaini ndiye Katibu wa chama
husika wilaya ya Mpwapwa.Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo alikubaliana na uamuzi
huo”
Aliongeza kuwa kamati za maadili kwa
ngazi ya jimbo na kata zinafanya kazi na kwamba hadi kufukia Januria 13 kamati
hazikupokea malalamiko yoyote kutoka kwenye vyama vinavyoshiriki uchaguzi mdogo
kata hiyo.
Alisema wanatarajia kutoa mafunzo kwa
makarani waongozaji na wasimamizi wa vituo vya kupigia kura tarehe 18 na 19
Januari na wameshaandaa vituo 12 vya kupigia kura vyenye wapiga kura 4123.
Kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi
wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe alisema hadi sasa kampeni zinafanyika kwa
kuzingatia taratibu za nchi na taratibu za uchaguzi na hakuna vurugu zozote
zilizojitokeza.
Hata hivyo aliwakumbusha wananchi
kuwa jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi na anaamini wasimamizi
wasaidizi wa uchaguzi wa kata na kamati za maadili zitawakumbusha wananchi
jukumu hilo.
Kwa upande
wa Msimamizi Msaidizi wa
Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi Bw. James Mkinga alisema maandalizi yote ya uchaguzi yamekamilika na
wameshabandika daftari la kudumu la wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura.
Mkurugenzi
wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe
aliwakumbusha wasimamizi wasaidizi kuhakikisha Sheria, kanuni na taratibu zote
za Uchaguzi zinazingatiwa.
Aliwataka wawakumbushe
wananchi kufika kwenye vituo vya kupigia kura kwa wakati ili kuepuka kukosa
haki ya kupiga kura kwa sababu ya kuchelewa kufika kituoni.
“Hakikisha
mnavikumbusha vyama vyote kuondoa mabango ya kampeni yaliyopo kituoni siku ya
kupiga kura na kama hawawezi kuyaondoa uwafahamishe kwamba utayaondoa kwa
sababu sheria inakataza” alisema Bw. Kawishe na kuongeza kuwa:
“Wakumbusheni
wasimamizi wa vituo kufuata Sheria, kanuni na taratibu na yeyote atakayekiuka
Sheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi haitasita kumchukulia hatua za Kisheria”
Aliwakumbusha
kuhakikisha kuwa mawakala wa vyama wanafuata taratibu zote inapotokea chama
kinataka kumbadilisha wakala kwenye kituo cha kupigia kura.
Naye
Mkuu wa Kanda ya Kati ya Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Saada
Kangeta aliwakumbusha wasimamizi wasaidizi kuwa iwapo litajitokeza jambo
linaloweza kuchelewesha matokeo kama kufanya uamuzi ya kura za mgogoro wawafahamishe
wananchi ili kuepuka vurugu
No comments:
Post a Comment