Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika
Makhtar Diop wakwanza kulia wavivuta kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu
ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji
la Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI
George Simbachawene pamoja na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi
pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene na Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati Makamu wa Rais
wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakwanza (kulia) akivuta utepe
kuashiria Ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya
Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka kadi ya
Kieletroniki katika Mashine ya UDART ilikuweza kupita kama ishara ya Ufunguzi
rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo
Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Pembeni yake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais –TAMISEMI George Simbachawene akimuelekeza jambo katika mashine hizo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa
Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop pamoja na viongozi wengine
wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na
Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye
mashine hizo mara baada ya uzinduzi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji
Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwa
wanahabari mara baada ya kuzindua utoaji huo wa huduma ya usafiri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akifurahia mara baada ya kuendesha gari la Mwendo Kasi
katika kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Haraka (BRT) mara baada ya kufungua
rasmi Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka
katika jiji la Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono
pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop mara
baada ya kutoka kukagua moja ya basi linalotumika katika utoaji huduma ya
Usafiri wa Haraka (BRT)
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo
pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakati
Msanii Mrisho Mpoto alipokuwa akitumbuiza.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop akimtunza msani Mrisho Mpoto wakati alipokuwa akitumbuiza katika kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Haraka BRT-Kariakoo huku Rais Dkt. Magufuli akifurahia.
PICHA NA IKULU














0 Comments