Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara
baada ya kuweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi
Mkoani Kagera.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe
kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani
Kagera. Wengine katika picha ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage,
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge
Vija Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Elimu Profesa
Joyce Ndalichako wakiwa wameshika utepe huo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili katika eneo la Ujenzi wa Kituo cha Afya cha
Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya
ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la mradi wa ujenzi wa
kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
Taaswira
ya moja ya jengo katika mradi huo wa kituo cha Afya cha Kabyaile kilichopo
Misenyi mkoani Kagera.
PICHA NA IKULU
........................................................................................................
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli leo Jumapili Januari Mosi, 2017 ameendelea na ziara yake ya
siku mbili Mkoani Kagera kwa kukagua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa
kituo cha afya cha Kabyaile kilichopo Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera
Akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla ya
uzinduzi wa kituo hicho cha Afya Rais Dkt Magufuli amesema serikali kwa sasa
imeweka nguvu kubwa katika kurejesha miundo mbinu ya huduma za jamii
iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10,2016 Mkoani humo
badala ya kujenga nyumba ya mwananchi mmoja mmoja.
''Na ndio maana
nimeona leo hapa tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka 2017 niwaeleze ukweli maana
kuna watu wanapitapita huko na wapo wengine nyumba zao zilibomoka kidogo
wakadanganywa wakaambiwa kuwa serikali itakuja kuwajengea nyumba wakazibomoa
zote ''waafwa'' kama ulitegemea ukiibomoa utalipwa fidia,hakuna''
Aidha Dkt Magufuli amemwagiza Waziri wa Nishati
na Madini Profesa Sospeter Muhongo kupeleka huduma ya umeme katika kituo hicho
cha afya alichokiwekea jiwe la msingi,ambapo pia ameahidi kutoa kiasi cha
shilingi Bilioni moja kwa ajili kutengeneza barabara inayoelekea kituoni hapo
kwa kiwango cha lami.
Pia ameuagiza uongozi wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) wanaojenga kituo hicho cha afya kuharakisha ujenzi wake na
kukamilika kabla ya mwezi februari badala ya Machi mwaka huu.
Dkt Magufuli ameutaka uongozi na wananchi wa
Wilaya ya Misenyi na maeneo mengine nchini kutumia vyema mvua chache
zinazonyesha mkoani humo kulima mazao yanayokomaa kwa muda mfupi ili kuepukana
na baa la njaa na kwamba serikali haina mpango wa kugawa chakula cha bure.
Jaffar
Haniu
Naibu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kagera.
01 Januari,
2017










0 Comments