Rais wa Uturuki, Mheshimiwa , Recep Tayyip Erdogan akiongozana na
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege
wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam kwa ziara rasmi Januari
22, 2017.Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John
Magufuli.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep
Tayyip Erdogan aliyefuatana na mkewe, Mheshimiwa Emine Erdogan (kulia)
wakifurahia ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage jijini Dar
es salaam baada ya Rais huyo kuwasili kwa ziara rasmi nchini Januari
22, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John
Magufuli.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan akiagana na Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kumfikisha kwenye hoteli ya Serena
jijini Dar es salaam baada ya kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Dar
es salaam na kumsindikiza hadi kwenye hoteli hiyo alikofikia Januari 22,
2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
...................................................................
RAIS
wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo jioni (Jumapili,
Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.
Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja
na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt Çavuşoğlu,
Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat
Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak
.
Pia
Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
2
MTAA WA MAGOGONI,
S.
L. P. 3021,
11410
- DAR ES SALAAM
JUMAPILI,
JANUARI 22, 2016.



0 Comments