Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura
(katikati) akielekea katika Ukumbi wa Utamaduni katika Chuo cha KumbuKumbu ya
Mwalimu Nyerere kufungua kongamano la Lugha ya Kiswahili. kulia ni Naibu Mkuu
wa Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere( Mipango Fedha na Utawala) Dkt.
Magreth Shawa na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo
vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Bw. Byatato Awadh
...........................................................................
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Serikali kupitia Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo imeanza rasmi kuandaa Sera ya Lugha ambayo itatoa
muongozo kwa taifa kuhusu masuala yote ya maendeleo ya Lugha nchini ikiwemo
Lugha ya Taifa ya Kiswahili.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura wakati
akifungua kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha
KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Anastazia Wambura
amesisitiza kuwa kwa kipindi kirefu sana kumekuwa na uhitaji wa Sera ya Lugha
ambayo itasaidia katika ukuaji na matumizi sahihi ya Lugha hasa Lugha ya Taifa
ya Kiswahili.
“Kwa hivi sasa rasimu ya awali
imeandaliwa na tunaendela kupokea maoni kutoka kwa wadau na kuyachambua”
Alisistiza Mhe. Anastazia.
Ameeleza kuwa Sera ya Lugha
itasaidia Lugha za Asilia, Lugha za
alama , maandishi ya nukta nundu na Lugha za kigeni kuwekewa mkakati wa
kuzishughulikia na kuzitumia kwa kukidhi mahitaji ya maendeleo endelevu ya
Taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Shani
kitogo ameeleza kuwa mchakato wa kupokea maoni unaendelea na amewaomba wadau wa
Lugha hasa Lugha yetu adhimu ya Kiswahili kuendelea kutoa maoni yao kwa ajili
ya kupata Sera ya Lugha iliyo bora na itakayosaidia katika maendeleo na ukuaji
wa Lugha nchini.
“Niwaombe wadau wa Lugha nchini
waendelee kuleta maoni yao kwetu ili kuweze kufanikisha kupata Sera ya Lugha
kwa Maendeleo ya Taifa Letu” Alisisitiza Bibi Shani.
Aidha Mwenyekiti wa Chama cha
wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Bw. Byatato
Awadh ameishukuru Serikali ya waamu ya Tano kupitia Wizara ya Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha wadau wa Lugha kwa kuanza
kuandaa Sera ya Lugha itakayoleta maendeleo katika ukuaji wa Lugha nchini.
“ Niishukuru Serikali ya Awamu
ya Tano kwa kuwa sikivu kwa wananchi na wadau wa maendeleo na tunaahidi kutoa ushirikiano
katika uandaaji wa Sera hii ya Lugha”Alisisitiza Bw Byabato.
0 Comments