Mkurugenzi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Prof. Martin
Valler Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Afya wa Chuo kikuu cha Witwatersrand cha
Nchini Afrika ya Kusini wakiangalia jinsi upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization)
unavyofanyika katika chumba Cath Lab kilichopo katika Taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea jinsi upasuaji wa Magonjwa ya Moyo unavyofanyika
katika taasisi hiyo wakati wageni kutoka
Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini walipotembelea wodi aliyokuwa amelazwa mmoja
wa wagonjwa aliyefanyiwa upasuaji. Kutoka kulia ni Prof. Martin Valler, akifuatiwa na Afisa
Muuguzi Roger Kibula, watatu kulia ni Prof. Simon Nemutandani na wa pili
kushoto ni Dkt. Marion Bergman.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaonyesha wageni kutoka Chuo kikuu cha
Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini sehemu ya malipo ambapo wagonjwa wanalipia
huduma. Wageni hao walitembelea Taasisi hiyo hivi karibuni ili kuona huduma za
matibabu ya moyo wanazozifanya pia
waliahidi kuimarisha mahusiano kati
yao hii ikiwa ni pamoja na kutoa
ufadhili wa masomo kwa madaktari wataokwenda kusoma katika chuo hicho.
Daktari
bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mhadhili
kutoka chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) Prof. Johnson
Rwakatare akimuonyesha vipimo vya moyo (ECHO) Prof. Martin Valler Mkuu wa
Kitivo cha Sayansi ya Afya wa Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya
Kusini alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete hivi karibuni.
Picha no. 6 Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akiwaeleza wataalamu wa afya kutoka Chuo Kikuu cha Minnesota cha nchini
Marekani huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa wakati walipoitembelea Taasisi hiyo hivi karibuni.
Picha na Anna Nkinda -
JKCI





0 Comments