Shughuli za ujenzi wa barabara za juu
(Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
Shughuli za ujenzi wa barabara za juu
(Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
Shughuli za ujenzi wa barabara za juu
(Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya ujenzi ya
Sumitomo Mitsui, Bw.Kiyokazu Tsuji (wa kwanza kulia) akionesha hatua
zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa Barabara za juu (Flyovers) eneo la
Tazara Jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni kiongozi wa timu ya ukaguzi wa
Miradi kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Omari Athuman.
Kiongozi wa timu ya ukaguzi wa Miradi
kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Omari Athuman (mwenye shati ya mikono mifupi)
akitoa ushauri kwa wahandari wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa bararabara za juu
jijini Dar es Salaam.
Mhandisi
Omari Athuman (kulia) akiongea na Ofisa Mshauri wa masuala ya usalama
kazini, Bw. Richard Barwan wakati wa
ziara ya Timu ya Mipango katika mradi wa ujenzi wa Barabara za juu eneo la
Tazara jijini Dar es Salaam.
........................................................................................
Na
Adili Mhina, Dar.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Tume ya Mipango imefanya ziara katika Mradi wa ujenzi wa Barabara
za juu (Flyovers) unaoendelea katika makutano ya barabara za Nyerere/Mandela Jijini
Dar es salaam na kuelezwa kuwa utekelezaji wake umefikia asilimia 19.2.
Ziara hiyo iliyofanyika hivi
karibuni kwa lengo la kuangalia maendeleo ya mradi huo ilitoa fursa kwa Bw.
Kiyokazu Tsuji, Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui
ambayo ndiyo inayotekeleza ujenzi huo kueleza maendeleo ya ujenzi kwa wataalam
kutoka Tume ya Mipango.
Mhandisi huyo alieleza kuwa
malengo ya awali yalielekeza kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Novemba 2016,
utekelezaji uwe umefikia asilimia 21.2 lakini lengo hilo halikufikiwa kutokana
na moja ya mashine kupata hitilafu na kulazimika kuagiza wataalam kutoka nje ya
nchi kuja kuifanyia matengenezo.
Hata hivyo Mkandarasi huyo
alieleza kuwa tayari wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanafidia muda
uliopotea wakati mashine hiyo ilipokuwa haifanyi kazi ili ujenzi wa barabara
hizo ukamilike ndani ya muda uliopangwa.
Nao walaalam kutoka Tume ya
Mipango walieleza kuwa Serikali na Wananchi kwa ujumla wanatarajia kuwa ujenzi
huo utakamilika kwa muda uliopangwa hivyo Mkandarasi huyo ana wajibu wa kufanya
kila linalowezekana ili mradi huo ukamilike kwa wakati.
Wataalamu hao pia walimshauri
Mkandarasi huyo kuwa ni vyema akawapeleka nje wataalam wanaoziendesha mashine
hizo ili waweze kupata ujuzi na uwezo wa kutengeneza mitambo pale inapohitajika
badala ya kusubiri watu kutoka nje kuja kufanya kazi hiyo.
Walieleza kuwa kuwepo kwa wataalam
wa ndani wenye uwezo wa kutatua hitilafu zinazojitokeza katika mitambo itasaidia
kupunguza gharama na kuokoa muda ili kufanya mradi uende bila kusimama.
Ujenzi huo unaotekelezwa kwa
miezi 35 kauanzia Disemba 1, 2015 hadi Oktoba 31, 2018 unalenga kupunguza tatizo la
msongamano wa magari na kuboresha huduma za usafiri katika Jiji la Dar es
Salaam.






0 Comments