Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) walipotembelea na Kukagua Mradi wa Umeme
uliopo moja ya kijiji kilichopo Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe.
Chiku Galawa (aliesimama) akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) pale kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua
miradi ya Umeme Songwe Vijijini, katika Kikao kilichofanyika leo katika Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa Mjini Songwe.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Livingstone Lusinde akifafanua
jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati hiyo, pale walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya wa Ileje tayari ya kwenda kukagua Mradi wa Umeme uliopo kijijini hapo, Kushoto
wake ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt. Medard Kalemani na Kulia
kwake ni Katibu Kamati wa Bunge anaehusika na Hesabu za Serikali (PAC) Ndg.
Asmin Kihemba na anaefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Joseph M. Mkude. katika
kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Ileje Mkoani Songwe.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Joseph
M. Mkude (aliesimama) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Hesabu za Serikali (PAC) pale kamati hiyo ilipomtembelea Ofisi kwake tayari kwa
Ukaguzi wa mradi wa umeme katika moja ya kijiji kilichopo Wilaya ya Ileje, Katika
kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
No comments:
Post a Comment