Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka . ................................................................................................. Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam |
Umoja wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesifu msimamo imara ulioonyeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujali na kupigania maslahi ya wananchi wanyonge hatimaye kuzuia mpango batili wa Tanesco kupandisha bei ya umeme nchini .
Pia Umoja huo umeelezea kufurahishwa kwao na kuunga mkono uamuzi huo ambao umethibitisha kuwa Dk Magufuli ni mtawala anayejali, kuthamini na kupigania maslahi ya wananchi wanyonge na wenye vipato vya chini.
Matamshi hayo yametakwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka mara baada ya kikao cha watumishi wa UVCCM kutathmini utendaji wa mwaka 2016 na kuweka mikakati ya utendaji kwa mwaka 2017 kilichofanyika katika ukumbi wa UVCCM makao makuu Upanga Dar Es Saalam.
Shaka alikitaja kitendo cha Rais Dk Magufuli kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco ) ameonyesha ujasiri, uzalendo na upendo kwa wananchi ambao walimpa dhamana ya kuongoza dola .
Alisema haiwezekani Bodi au Menijmenti ya Tanesco ifikie hatua ya kuamua au kupitisha maamuzi mazito ya kitaifa na kupandisha bei ya umeme bila ya Waziri dhamana wa Wizara ya Serikali asijulishwe .
"Tuko pamona na Dk Magufuli , tunampa mkono wa heko kuzuia kupanda bei ya umeme , ametazama maslahi mapana ya wanabchi , hali za watu wanyonge na wenye vipato vya chini, ametetea maslahi ya waliomuweka madarakani"Alieleza Shaka.
Aidha alisema Tanesco kwa kupitia Mkurugenzi wake na Waziri mwenye dhamana waliwaahidi wananchi kwamba bei ya umeme katu haitapenada hivyo bei kama ingependa na serikali kukaa kimya ingalikuwa ni kituko cha mwaka.
Kaimu katibu mkuu Shaka aliwataka watendaji wa serikali , wakurugenzi wakuu wa mikoa, wajumbe wa bodi makamishna, makatibu wakuu na wakurugenzi wa halamshauri za wilaya waendelee kutekekeza majukumu yao kwa mujibu wa mipaka yao, taratibu na shera bila kukurupuka.
"Watumishi na watendaji wenye dhamana wakae wakijua mambo yamebadilika, zama hii si zama zile zilizopita, Dk Magufuli na serikali yake ni makini huku wakifuatilia kila pembe, atakayevimbisha mashavu ya ukaidi si ajabu akatubuliwa" Alisisitiza Shaka
Hata hivyo UVCCM imewahimiza watendaji na watumishi wa serikali waliopa katika sekta za maendeleo kusoma upepo, kutenda haki na kutimiza wajibu na kwamba maamuzi wanayopanga kuyapitisha ni lazima kwanza yajali maslahi ya Taifa.
Shaka alifafanua kuwa ni vyema ikafahamika na kueleweka kwamba Serilkali ya Chama cha Mapinduzi imebeba imani, mioyo, matumaini na maisha ya watu hivyo umma wakati unapokitegemea CCM , anapotokea mtu mmoja akaamua kuvuruga utaratibu heri mtu huyo akawekwa pembeni.
"Tunaipongeza Serikali ya CCM kwa kuendelea kusimamia nidhamu ya kazi, kupigania dhana ya utumishi wa umma , uwajibikaji , uwazi pia kukomesha vitendo vya rushwa, maonevu na ufisadi , tunamshauri Dk Magufuli aendelee kusimamia majukumu yake bila kutikisika "Alisema Shaka
Alimaliza kwa kuusema huku akiwataka watendaji dhamana kujipanga kimkakati na kimipango kwa lengo la kutimiza ahadi zote zilizoanishwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2015 /2020 kwa sababu huo ndiyo mkataba kati ya wapiga kura na Serikali ya CCM.
No comments:
Post a Comment