
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu Mwenyeiti wa CCM (Bara)
Philip Mangula baada ya kuwasili kwenye jengo la Halmashauri ya Wilaya
ya Wanging'ombe kufungua jengo hilo Januri 21, 2017. Mangula ni mkazi wa
eneo hilo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa Kiwanda
cha Chai cha Kibena wilayani Njombe baada ya kukitembelea Januari 21,
2017.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua jengo la Ofisi za Halmashauri ya Wilaya
ya Wanging'ombe katika eneo la Igwachanya Januari 17, 2017. Kushoto
kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Wanging'ombe baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo hilo katika eneo
la Igwachanya , Januari 17, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha chai cha Kibena wilayani Njombe Januari 21, 2017.

Waziri
Mkuu, Kasisim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa eneo la Igwachanya
wilayani Wanging'ombe baada ya kuweka jiwe la msingi la Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya hiyo Januari 21, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ilembula wilayani Wanging'ombe Januari 21, 2017.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya wasanii wa eneo la Wikichi
wilayani Njombe wakati alipowasili kwenye eneo la Mradi wa Ujenzi wa
Hospitali Mpya ya Rufaa ya Mkoa huo, Januari 21, 2017.Kushoto kwake ni
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher `Ole Sendeka.
..................................................................
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema jumla ya vijiji 53 vya mkoa wa Njombe
vitapatiwa huduma ya maji safi na salama katika mwaka huu wa fedha.
Alitoa
kauli hiyo jana (Jumamosi, Januari 21, 2017) wakati akizungumza na
wananchi wa wilaya ya Wanging’ombe katika mkutano wa hadhara katika kata
ya Ilembula.
Waziri
Mkuu alisema zaidi ya sh. bilioni 2.4 zimetengwa kwa ajili ya
kugharamia mradi huo wa maji katika miji ya Makambako, Njombe na wilaya
ya Wanging’ombe.
Alisema
kati ya vijiji hivyo vitakavyopatiwa maji, vijiji 22 ni vya wilaya ya
Wanging’ombe, hivyo aliwaomba wananchi hao kuwa na subira.
Kwa
mujibu wa Waziri Mkuu tayari zabuni ya mradi huo imeshatangazwa, hivyo
amewaagiza viongozi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji watafute mkandarasi
mzuri.
Alisema
lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kila mwananchi
anapata huduma ya maji katika umbali usiozidi mita 400 kutoka mahali
anapoishi.
Waziri
Mkuu alitoa kauli hiyo baada ya Mbunge wa Wanging’ombe, Mheshimiwa
Mhandisi Gerson Lwenge kumuomba awasaidie katika kutatua kero ya maji.
Mbunge
huyo ambaye pia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji alisema “Mheshimiwa
Waziri Mkuu sisi tunakabiliwa na changamoto ya maji, leo tunaomba
ututatulie kero hii”.
Changamoto
nyingine aliyoitaja Mheshimiwa Lwenge ni pamoja na ukosefu wa hospitali
ya wilaya, ambapo Waziri Mkuu aliigiza halmashauri hiyo kuanza ujenzi.
Alisema
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 inaelekeza kuwa na
hospitali katika kila wilaya, kituo cha afya kwa kila kata na zahanati
kwa kila kijiji.
Katika hatua nyingine
Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Ally Kasinge kukutana na
viongozi wa kata na vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Mapanga Kipengele
ili kutatua kero ya mpaka.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JANUARI 22, 2017.
0 Comments