...................................................................................................................
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt. Medard Kalemani (aliesimama)
akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC) pale kamati hiyo ilipofanya ziara katika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Iringa wakati walipokuwa wakisoma taarifa za Utekelezaji Miradi
ya Umeme Vijijini katika Kikao kilichofanyika leo Iringa Mjini. Kulia
kwake ni Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe.Livingstone Lusinde
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.
Japhet Hasunge akizungumza mbele ya kamati hiyo pale kamati ilipofanya
ziara katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa wakati
walipokuwa wakisoma taarifa za Utekelezaji Miradi ya Umeme Vijijini
katika Kikao kilichofanyika leo Mjini Iringa.
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.
Livingstone Lusinde akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari idodi
iliyopo Iringa Vijijini pale kamati hiyo ilipoenda kukagua Miradi ya
Umeme Vijijini kwa kuwa Shule hiyo ni moja ya wanufaika wa miradi hiyo.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)



0 Comments