Kamishna Msaidizi- Nishati
Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (wa
kwanza kulia) pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na
Madini wakiwa katika kivuko cha kuelekea katika Wilaya ya Ukerewe, Mwanza kwa
ajili ya kukagua miradi ya umeme jua inayotekelezwa na kampuni ya Rex Energy.
Kamishna Msaidizi- Nishati
Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila
(kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis
Kibhisa (kulia) katika ziara hiyo.
Kamishna Msaidizi- Nishati
Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kulia)
akibadilishana mawazo na Afisa Sheria kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Peter
Malendecha (kushoto) mara baada ya kuwasili katika wilaya hiyo.
Kamishna Msaidizi- Nishati
Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kulia
nyuma) pamoja na wajumbe wengine
wakielekea katika kisiwa kidogo cha Ghana/Siza kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme jua inayotekelezwa
na kampuni ya Rex Energy.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis Kibhisa
(kulia) akielezea hatua ya utekelezaji ya miradi ya kusambaza umeme katika
kisiwa cha Ghana/Siza wilayani Ukerewe kwa Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka
Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto)
Sehemu ya miundombinu ya umeme
iliyokamilika katika kisiwa cha Ghana/Siza
Katibu wa Kitongoji cha
Ghana/Siza wilayani Ukerewe, Frank
Matondane akielezea mahitaji ya umeme
katika kitongoji hicho mbele ya Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara
ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila pamoja na wataalam kutoka Idara
ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani)
Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis
Kibhisa (kushoto) akionesha eneo litakalowekwa mitambo ya umeme katika kitongoji cha Ghana/Siza wilayani Ukerewe kwa Kamishna
Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden
Rwebangila (kulia).
No comments:
Post a Comment