Bondia Meshack Mwankemwa wa MbeyaPicha na SUPER D BOXING NEWS
.................................................
|
Na Mwandishi Wetu
Bondia
Meshack Mwankemwa wa Mbeya ameingia jijini Dar es salaam kwa ajili ya
mpambano wake na Ramadhani Shauri mpambano utakaokuwa wa raundi kumi za
ubingwa wa EAST/ CENTRAL AFRICA siku ya Feb 5 katika uwanja wa ndani wa
Taifa mpambano wa raundi kumi
akizungumza
na wahandishi wa habari Promota wa mpambano uho Sadick Kinyogoli
amesema kuwa huu ni wakati wa mwisho wa kuelekea mpambano wenyewe mana
utafanyika mwishoni mwa wiki hii
aliongeza
kwa kusema Mwankemwa ametuwa jijini tangu mwishoni mwa wiki iliyopita
na Shauri ndio kwao hivyo mpambano utakuwa mkali sana kwa kuwa mabondia
wote wameshacheza mapambano makubwa ya kimataifa hivyo wapenzi waje
mapema kuangalia burudani ya mchezo wa masumbwi walioikosa kwa kipindi
cha nyuma
katika mpambano huo pia kutakuwa na mapambano mengine ya kusindikiza mtanange uho
Kinyogoli
alisema kuwa bondia Mohamed Matu,mla atapambana na Mfaume Mfaume wakati
bondia chipkizi anaekuja kwa kasi katika mchezo uhu wa masumbwi Iddi
Mkwela ataoneshana umwamba na Manyi Issa mpambano wa raundi kumi
zisizokuwa na ubingwa
mchezo
mwingine wa ubingwa wa taifa utakuwa kati ya Said Chino na Twalib Tuwa
ubingwa wa taifa wa TPBC mkanda ambao unatetewa na Tuwa Husein Pendeza wa Ashanti Boxing clab ya Ilala atakaevaana na Said Hamdani kutoka Mbezi Conetion na Mbwana Matumla atazichapa na Suleimani Shabani
pamoja na mpambano mwingine wa kimataifa wa kina dada Anisha Bashir kutoka Malawi na Ester Boazi Kazeba wa Tanzania
aliongeza
kwa kusema kuwa mabondia wote watapima uzito pamoja na Afya zao siku ya
feb 4 katika hotel ya Atrium iliyopo sinza Afrika sana hiyo mabondia
wote watakuwa pale jumamosi kwa ajili ya upimaji uzito pamoja na Afya
zao
0 Comments