
| Mwanzilishi wa Divine Worship Joshua Ngoy Ngoy ama wengine wanavyomfahamu kama Joshua music kama anavyoonekana hapo pichani . |
Na.Veo Ignatus Arusha/Kilimanjaro
Divine
Worship imejiandaa kutembelea kituo cha watoto yatima na wajane
kilichopo Manispaa ya Moshi mjini Mkoani Kilimanjaro kiulikanacho kama
Kitaa Hope Children Home wakiwa na lengo la kuwatembelea na
kuzifahamu changamoto mbalimbali wanazopitia watoto hao pamoja na
wakina mama hao wajane .
Hayo
yamesemwa na mwanzilishi wa kundi la Divine Worship
Joshua NgoyNgoy
ambapo amesema kuwa wameamua kutenga siku maalumu kukitembelea kituo
hicho ili kuwaonyesha upendo kwa watoto hao, ili na wao wajisikie ni
binadamu wengine"tutakaa nao,tutakula nao pamoja ikiwezekana hata
kucheza nao kwa pamoja ili na wao wajisikie faraja na kuwa jamii
inawakumbuka pia"
Aidha
amesema kuwa hawa watoto yatima na wao wanahitaji kujisikia vizuri
kama watu wengine wanavyojisikia.
"Yatima
hawa na wajane wanatamani na wao wawe na maisha mazuri kama yale
unayoishi wewe hivyo basi tuungane kwa pamoja kwenda kuwatembelea watoto
hawa ,ukiwa na chakula ,mavazi,,pesa kiasi chochote tuungane kwa pamoja
tukawatembelee naomba sapoti yenu kukitembelea kituo hichi,kwani jambo
kama hili tukifanya kwa moyo linampa Mungu utukufu" alisema Joshua.
Amesema
siku ambayo wameitenga ni tarehe 18 februari ambapo itakuwa siku ya
jumamosi saa nne asubuhi, hivyo amewaomba watanzania wote ,makampuni
mbalimbali pamoja na wadau mabalimbali ili kuwasaidia watoto hawa pamoja
na wajane waliopo kituoni hapo.
![]() |
| Muanzilishi wa Huduma ya Divine Worship akiwa katika moja ya ibada kama inavyoonekana pichani |
Sambamba
na hayo Joshua amesema kuwa ifikapo juni mwaka huu wanatarajia kufanya
tamasha la shukurani (thanks giving)tangia kuamnzishwa kwa
huduma hiyo ya Divine Worship inayohusika na kuandaa ibada halisi ya
kumsifu Mungu.
Aidha
amesema kuwa huduma hiyo ilianzishwa 26june2016 ikiwa na lengo la
kuwaunganisha waimbaji pamoja na wapigaji vyombo mbalimbali wakiwa na
lengo moja la kumsifu Mungu kwa kila mmoja kwa nafasi yake bila kujali
madhehebu wala kabila la la mtu ili hali tu ni kiungo katika mwili wa
Kristo.
![]() |
| Muanzilishi wa Divine Worship akiwa anafuatilia jambo kwa makini katika mojawapo ya Ibada |
![]() |
Baadhi
ya waimbaji wa huduma ya Divine Worship wakiwa jukwaani
wanaimba.


Waimbaji wa huduma ya Divine Worship Kama wanavyoonekana
pichani wakihudumu .
Amesema
kuwa mwaka huu wamejipanga kivingine wanayo malengo nya kufikia
Tanzania yote na nje ya nchi kwaajili ya kumsifu Mungu, kuwafikia watu
wa rika zote.
"Hatusemi
hakuna watu wanaomuabudu Mungu katika roho nakweli wapo na wapo
waliotutangulia na tunawaheshimu, ila kila mmoja anafanya kwa namna
ambayo Mungu amemuagiza kufanya bila kumbagua mu yeyote yule ilihali
akijua anafanya kwaajili ya kumsifu na kumtukuza Mungu na wala siyo kwa
matakwa yake wala mwanadamu yeyote yule"alisema.
Hadi
sasa tangia kuanzishwa kwa huduma ya Divine Worship mwaka jana 2016
tayari wameshafanya ibada mbili ambapo itakapofika june mwaka huu
watakuwa wametimiza mwaka mmoja katika huduma hiyo.



0 Comments