Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Bagamoyo, alhaj Abdul Sharif akizindua umeme kwa niaba ya wazazi katika shule ya sekondari Kingani .
(picha na Mwamvua Mwinyi)
Katibu wa mbunge Jimbo la Bagamoyo Magreth Masenga akipokea cheti cha shukuru kwa niaba ya mbunge Dk. Shukuru Kawambwa kutokana na kusaidia kutatua tatizo la ukosefu wa umeme shule ya sekondari Kingani.
(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Bagamoyo, alhaj Abdul Sharif, akitoa shukrani kwa mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dk.Shukuru Kawambwa kwa niaba ya wazazi wa shule ya sekondari Kingani baada ya kutatua kero ya ukosefu wa umeme shuleni hapo.
(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Kingani kata ya Kisutu, Bagamoyo akizungumza na wazazi wa wanafunzi shuleni hapo kuhusu mafanikio na changamoto zinazowakabili.
(Na Mwamvua Mwinyi)
.................................................................................
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo ,Dk.Shukuru Kawambwa,ametatua kero ya ukosefu wa umeme katika shule ya sekondari ya kingani ,kata ya Kisutu,kwa kugharamia zaidi ya mil.17 hivyo tatizo hilo kwasasa kubakia historia.
Wanafunzi na walimu shuleni hapo ,wameanza kunufaika umeme wa uhakika kutoka Tanesco baada ya kuteseka kwa kipindi kirefu bila kupata huduma hiyo.
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Kingani,Method Kunambi,aliyasema hayo wakati akizungumza na wazazi wa wanafunzi shuleni hapo,kuhusu maendeleo ya shule na changamoto zinazowakabili.
Alieleza kuwa nishati hiyo ina mchango mkubwa kwa wanafunzi ili waweze kujisomea nyakati yoyote ili kukuza taaluma zao.
Alisema tatizo hilo lilidumu kwa miaka nane tangu waanze kufanya mchakato wa kuomba kupata umeme mwaka 2007.
Kunambi alisema,shirika la umeme Tanesco lilihitaji kiasi cha sh.mil.15,513,811.6 kwa ajili ya transformer,upatikanaji wa umeme ambapo walishindwa kumudu kulipia gharama hizo.
“Mwaka 2014 jitihada zetu ziligonga mwamba na kushindwa kupata wadau kabisa wa kutusaidia,ambapo mbunge alijitokeza kutusaidia kulipia gharama za transformer na service line mi.13.569.845.65 kupitia mradi wa REA “
“Gharama hizo hazikutosha kupata umeme shuleni mwaka 2016 hiyo ,dk.Kawambwa kupitia mfuko wa jimbo alilipia gharama zilizobakia mil.3,458.468 na sasa tumeingiziwa umeme”alisema mwalimu Kunambi.
Hata hivyo Kunambi,alieleza licha ya kumaliza tatizo hilo lakini bado wana tatizo la uhaba wa viti 77 na meza 107 kwa wanafunzi, viti 38 na meza 38 kwa walimu ,nyumba za walimu 59 ,madarasa, maabara na hosteli za wavulana nne.
Akishukuru kwa niaba ya wazazi ,mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Bagamoyo,alhaj Abdul Sharif,alisema mbunge huyo kaonyesha ujali na kuvalia njuga suala hilo muhimu.
Alisema umeme huo utasaidia wanafunzi watasoma kwa vitendo,walinzi wataweza kulinda kwa usalama zaidi na walimu kufanya kazi zao kiufanisi.
Alhaj Sharif ,alisema ni viongozi wachache wa kuchaguliwa ambao wana moyo wa kujitolea fedha zao kwa ajili ya jamii hivyo dk.Kawambwa anastahili pongezi kubwa.
Nae katibu wa mbunge wa jimbo la Bagamoyo,Magreth Masenga akizungumza kwa niaba ya dk.Kawambwa alipokea shukrani zilizotolewa na walimu na wazazi shuleni hapo.
Magreth alisema ,mbunge huyo ataendelea kusimamia kero zinazowakabili wananchi ili kuhakikisha maendeleo ya jimbo yanapiga hatua.




0 Comments