FILAMU ZA KIBONGO
KUTETEMESHA TUZO ZA DStv AFRICA MAGIC VIEWERS’ CHOICE 2017
Dar es Salaam Jumatano Februari 1,
2017; Wakati filamu
zitakazochuana katika tuzo za mwaka huu za Africa Magic
Viewers’ Choice(AMVCAs) zikitangazwa, filamu kutoka Tanzania zimeibuka katika
Makundi
matatu
tofauti kitendo kinacholeta matumaini ya kuona makubwa ya watanzania kuwika
kwenye tuzo hizo
zitakazofanyika katika jiji la Lagos nchini Nigeria mnamo mwezi Machi 2017
Filamu za
Kitanzania zinawika katika kundi la Filamu Bora kabisa Afrika Mashariki ambapo
kati ya filamu tano
zilizoteuliwa, tatu ni za kitanzania ambazo ni
“Aisha” ya Amil Shivji, “Naomba
Niseme” ya Staford
Kihore, na
“Homecoming” ya Seko Shamte.
Kundi jingine
ambalo filamu za Tanzania zimejitokeza ni lile la Filamu Bora za lugha ya
Kiswahili ambapo tamthilia ya
“Siri ya Mtungi” awamu ya pili ya John,
Louise na Jordan Riber imeteuliwa kushiriki
Kwenye kundi
kubwa la Sinema Bora kabisa barani Africa mwaka 2016, sinema mbili kati ya sita
zilizomo katika kundi
hilo ni za Tanzania ambazo ni “Aisha”
ya Amil Shivji na “Naomba Niseme” ya
Staford
Kihore.
Upigaji wa
kura kupendekeza washindi unaendelea hadi februari 24 ambapo utafungwa rasmi na
hafla ya kutangaza
washindi itafanyika tarehe 5 Machi 2017. Upigaji kura unafanyika kwa njia ya
mtandao na
pia mpigakura
anaweza kutembelea www.africamagic.tv au www.dstv.com ambapo ataweza kupelekwa moja kwa moja
kwenye ukurasa wa kupigia kura.
Akizungumzia tuzo hizo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande, amewasihi watanzania kupiga
kura kwa wingi ili kuwawezesha washiriki wetu kuibuka washindi. Amesema kwakuwa
washiriki ni wengi na wanatoka nchi mbalimblai kote Afrika, ni uzalendo pekee
wa kuwapigia kura watanzania wenzetu ndio utakaowahakikishia ushindi.
“Sasa Ni Zamu yetu” alisema Maharage
na kuongeza “Kitendo cha kazi za hawa watanzania kuingia kwenye mchuano,
kinamaanisha kazi zao zina ubora unaokubalika, hivyo inabidi tuwaunge mkono kwa
kuwapigia kura nyingi kadiri iwezekanavy. Watanzania watambua kuwa sasa ni zamu
yetu, na sisi tuuonyeshe ulimwengu kuwa tunaweza” alisema.
Tanzania ina rikodi nzuri kwenye tuzo hizi kwani msimu uliopita filamu
ya Kitendawili ya Richard Mtambalike ilinyakua tuzo ya filamu bora tya lugha ya
Kiswahili wakati Elizabeth Michael ‘Lulu’ alivuma katika tuzo hizo katika
filamu yake ya Mapenzi iliyoteuliwa kuwa filamu bora kabisa Afrika Mashariki.
Africa
Magic Viewers' Choice Awards (AMVCA) inafanyika kila mwaka na inaandaliwa na Multichoice Africa ikiwa na lengo la kutambua na kuthamini
mafanikia makubwa katika sekta ya filamu na televisheni
kulingana na
uchaguzi wa watazamaji.
0 Comments