- Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Abdulkadir Mohamed (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa pili kulia) shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Kampuni hizo Mwiba Holdings na Tanzania Game Trackers pia zimekubali kusaidia mabati 1000 ikiwa ni msaada. Wengine ni viongozi mbalimbali walioshiriki katika tukio hilo.
- Mkurugenzi
wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Pratik Patel akizungumza katika
tukio la kampuni hiyo kukabidhi shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa
ni jitihada za kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa shule za sekondari
wilayani Meatu. Kampuni hizo yaani Mwiba Holdings pamoja na Tanzania
Game Trackers pia zimekubali kusaidia mabati 1000 kama msaada.
- Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Abdulkadir Mohamed (kulia) akimtamkia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto) kuwa mbali na kampuni hiyo kutoa mifuko 3000 ya saruji kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Wataongeza msaada wa mabati 1000. Wengine ni Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa FCF, Pratik Patel (wa pili kulia) wakishuhudia tukio hilo.
Na Mwandishi Wetu, Simiyu
KAMPUNI kitalii
zilizo chini ya Friedkin Conservation Fund (FCF) Tanzania iliyowekeza
katika pori la Makao wilayani Meatu na Maswa Mkoani Simiyu imechangia
mifuko 3000 ya saruji na mabati na 1000 kusaidia ujenzi wa shule za
sekondari wilayani humo.
Misaada
hiyo yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 70 imetolewa na kampuni hizo
ikiwa ni kuunga mkono mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk.
John Magufuli kuendeleza elimu ya hasa katika maeneo ya wafugaji ambako
kampuni hizo zinafanya shughuli za uwindaji wa kitalii.
Kampuni
zilizokabidhi misaada hiyo juzi katika sherehe zilizofanyika mjini hapa
ni pamoja na Mwiba Holdings na Tanzania Game Trackers ambazo kwa pamoja
zimetoa saruji hiyo yenye thamani ya sh milioni 48 na mabati yakiwa na
thamani ya sh milioni 25.
Vifaa
hivyo vya ujenzi vitatumika kujenga vyumba vya madarasa na mabweni kwa
ajili ya shule zitakazotumiwa na watoto wa jamii za wafugaji zinazoishi
jirani na maeneo ya shughuli za uwindaji wa kitalii wilayani Meatu
katika mkoa wa Simiyu.
- Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto) akifurahia tamko la Mkurugenzi, Abdulkadir Mohamed (hayupo pichani) kuahidi kuongeza msaada wa mabati 1000 huku Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack akikabidhiwa kipaza sauti kurudia kauli ya neema za mabati 1000 toka FCF.
- Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meatu (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni ya FCF kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka pamoja na Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack.
Akizungumza
kabla ya kumkabidhi mchango huo Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka,
wakati wa hafla iliyofanyikia katika viwanja vya stendi Mjini Mwanhnuzi,
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Abdulkadir Mohamed alisema kuwa mchango huo
unatokana na kuanzishwa kwa mfuko uwekezaji katika pori hilo.
"Tunatoa
msaada huo ikiwa ni kuunga mkono Serikali yetu ya awamu ya tano katika
jitihada za kuimarisha sekta ya elimu nchini,na tumeanza kuwasaidia
wananchi tunaoshirikiana nao katika shughuli za uhifadhi na huu ndio
mwanzo wa kuendeleza ushirikiano huu ikiwa ni sehemu ya mchango wetu kwa
jamii,” alisisitiza Mkurugenzi huyo
Alisema
kuwa pamoja na kuchangia misaada hiyo,kampuni yake imekuwa ikitoa
misaada katika vijiji tisa vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi za Wanyama
Pori Makao (WMA) na ranchi ya Mwiba hasa katika kusaidia uboreshaji wa
huduma za jamii na hasa elimu.
“
Mpaka sasa Kampuni kupitia makampuni yake matatu tayari wamechangia
kiasi cha sh Milioni 3000 kwa vijiji tisa pamoja na vingine 15
vinavyopakana pori hilo, ambapo shule, zahanati, pamoja na vituo vya
maendeleo vimejsengwa katika vijiji hivyo kwa kushirikiana na
halmashauri” Alisema Mohamed.
Aidha,
aliongeza kuwa mchango huo umechangiwa na mafanikio mazuri ya shughuli
za utalii zinazoendelea katika maeneo hayo na uwekezaji wa kampuni hiyo
wilayani humo, huku akibainisha kuwa shughuli hizo zinazidi kupanda kila
mwaka wilayani humo
- Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiongozana na wageni wake katika hafla hiyo.
- Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack akijitambulisha katika hafla ya FCF kukabidhi shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu.
Mkurugenzi
huyo aliahidi kuwa kutokana na kuimarika kwa shughuli hizo na kuwepo
kwa mazingira mazuri ya uwekezaji,hasa ushirikiano wanaoupata kutoka kwa
wananchi, hasa wavijiji vinavyopakana na pori hilo, wamepanga kuongeza
uwekezaji wao kwa dola za kimarekani milioni 100.
Kwa
upande wake Mbunge wa Viti maalum Mkoa (CCM) Leah Komanya alipongeza
mchango wa mwekezaji huyo, huku akiunga mkono kwa kuchangia mabati 50
kwa ajili ya ujenzi wa mabweni shule ya sekondari Makao.
“
niwaombe hawa wawekezaji wetu wasichangie kwenye vijiji hivyo tisa peke
yake, bali wachangie hata kwenye kata nyingine za wilaya yetu ambayo
ipo chini sana kielimu ili kila mwananchi atambue mchango wao, na
niwapongeze kwa kuunga mkono ujenzi wa shule hasa mabweni kwa watoto wa
kike” Alisema Komanya
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, akizungumza kabla ya kupokea msaada huo, alimtaka
Mkurugenzi huyo ambao alidai kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro ya kila
mara kati ya wananchi na kampuni hiyo ili kurejesha imani ya kuendelea
kushirikiana na wawekezaji hao.
Mbali
na hilo Mtaka alipongeza Kampuni hiyo kwa mchango wake, huku
akielelekeza saruji hiyo pamoja na mabati vitumike kwa ajili ya kujenga
mabweni katika shule za sekondari zinazopakana na pori hilo.
Mtaka
aliwataka wawekezaji hao kuwa karibu na wananchi kwa kushirikiana na
watendaji wa halmashauri na alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya hiyo kuwapatia kiwanja cha kujenga ofisi ili iweze
kuratibu kwa karibu ushirikiano huo na wananchi.
Kwa
sasa mgogoro uliodaiwa kuwapo kati ya mwekezaji huyo na wanakijiji wa
Makao, umemalizika baada ya msuluhishi aliyeteuliwa na pande zote mbili,
Jaji Thomas Mihayo, kutoa uamuzi hivi karibuni baada ya walalamikaji
kushindwa kuwasilisha utetezi wao kwa wakati.
Hata
hivyo, taarifa zimeeleza kwamba hali hiyo imetokana na kurejea kwa
mahusiano kati ya pande hizo mbili na kuonekana njia bora zaidi ya
kusuluhisha migogoro ni mazungumzo yasiyo na gharama zinazoweza
kuigharimu serikali ya kijiji na wilaya
0 Comments