Mkoani Mwanza, Moses Mjuni na kufariki dunia papo hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Khadija Nyembo amesema kuwa ajali hiyo
imetokea saa mbili usiku ambapo Gari la Mbunge huyo lilimgonga Mtumishi
wa Hospitali ya Magu ambaye alikuwa anaendesha pikipiki na dereva wa
gari hilo teyari ameshakamatwa na Jeshi la Polisi.
Aidha, kwa upande wake, Esther Matiko amesema kuwa ajali hiyo
imetokea takribani kilomita 10 kutoka daraja la Mto Simiyu wakati
akitokea Mwanza.
“Nilitoka Mwanza saa 12:00 jioni kwenda Jimboni kwangu (Tarime),
tulipopita mbele kidogo karibu kilomita 10 kutoka Daraja la Mto Simiyu,
ghafla alitokea mwendesha pikipiki akiwa ana yumba yumba na dereva
alishindwa jinsi ya kumkwepa akamgonga, mimi nilikuja kuona yule mtu
teyari ameshakufa,”amesema Mtiko.
Hata hivyo, Matiko amesema kuwa alikuwa anajisikia maumivu makali ya
mgongo na mbavu hali ambayo ilimlazimu kufanyiwa vipimo kuona kama
amepata madhara.

0 Comments