Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Seleman S.Jafo akizungumza na walimu,
wanafunzi na Kamati ya shule ya msingi Chang’ombe A Manispaa ya Dodoma
alipofanya ziara kujionea maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao
umekamilka kwa asilimia mia moja. Kulia kwake ni Kaimu Afisa Elimu Mkoa Dodoma
Bw. Tumsifu Mwasamale na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Nelly kinyaga kushoto
kwake ni Diwani Kata ya Chang’ombe Mhe.Bakari Samweli Fundikira
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Seleman S.Jafo akifungua mlango ili
kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao umekamilika kwa asilimia mia moja
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Seleman S. Jafo akitoa agizo kwa
halmashauri, kamati za shule na mikoa nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea na
badala yake kutumia juhudi na maarifa ili kuwaletea wananchi maendeleo kwa
haraka. Ameridhishwa na ubora na kasi waliyoitumia kujenga majengo hayo
Mojawapo
ya madarasa yaliyokamilika katika shule ya msingi Chang’ombe A Manispaa ya
Dodoma. Jumla ya vyumba vya madarasa sita vimejengwa ili kukabiliana na
changamoto ya vyumba vya madarasa katika shule hiyo inayotokana na wingi wa
wanafunzi, shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 2000
.......................................................................
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo ametoa pongezi kwa utekelezaji wa agizo alilolitoa tarehe 03 Nov 2016 kwa uongozi wa
Halhamashauri ya Manspaa ya Mji wa
Dodoma alipofanya ziara ndogo katika
kata hiyo na kubaini changamoto mbalimbali katika shule ya msingi ya Chang’ombe
A .
Mhe. Waziri ametoa pongezi hizo kwa uongozi wa Halmashauri ya Manispaa , kamati ya shule ya Chang’ombe
,walimu na Diwani wa Kata ya Chang’ombe leo,
alipotembelea shule hiyo kukagua utekelezaji wa agizo juu ya kukamilika kwa ukarabati wa miundombinu katika
shule hiyo ifikapo 10 januari ambapo ameridhishwa kwa hatua nzuri
ya ukarabati huo.
‘’Maagizo niliyoyatoa
yalikuwa magumu sana lakini nia yangu ilikuwa kuwatengenezea mazingira
rafiki wanafunzi na walimu , nimefarijika na utekelezaji wake, hali
haikua nzuri hapo mwanzo lakini nimefarijika kwa kazi nzuri, muonekano wa madarasa
unaridhisha nawapongeza sana’’ aliongeza kwa kutoa pongezi kwa SUMA JKT kwa
kukamilisha kazi kwa wakati na katika kiwango stahiki.
Pia Mhe. Suleman Jafo amewataka wanafunzi na walimu wa shule ya
msingi ya Chang’ombe kutunza na kuitumia
miundombinu hiyo rafiki ili kuongeza ufaulu katika shule hiyo na kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa shule nyingine
.
Kwa upande wake Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo Bi. Nelly
Kinyaga ameishukuru serikali kwa
kuboresha miundombinu ya shule hiyo ambapo awali mazingira ya shule hiyo yalikuwa
sio rafiki kwa wanafunzi na walimu kutokana na
upungufu wa matundu 20 ya vyoo na
vyumba vya madarasa 8.
‘’ kwakweli kulikua na
changamoto sana wanafunzi walikua wengi na madarasa machache lakini kwasasa hatuna watoto wanaokaa chini
na msongamano wa wanafunzi darasani umepungua kwa kiasi kikubwa ,naishukuru serikali na Mhe. Jafo kwa kutilia
mkazo ukarabati wa miundombinu ya shule
yetu’’ alisema
Ally Mohamed Swalehe mmoja
wa wanafunzi wa shule ya Msingi Chang’ombe
ameishukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule hiyo rafiki kwakuwa itaongeza ufaulu katika mitihani na kuepusha magonjwa ya milipuko shuleni hapo.
Mhe. Waziri alitoa agizo hilo Tar 03 Nov alipofanya ziara ndogo ya kutembelea Kata
ya Chang’ombe ambapo katika ziara hiyo
alitoa agizo kwa Halhamashauri ya Manispaa ya Dodoma kuhakikisha
inakamilisha ujenzi wa matundu 20 ya vyoo na vyumba vya madarasa 8 pamoja na ukarabati wa vyumba vya madarasa 2 katika shule ya Chan’gombe A ifikapo tarehe 10 januari 2017 kabla ya msimu
wa masomo kuanza.




0 Comments