
Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya
hafla fupi ya utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la
Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika
ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari
cha Gereza Mbigiri – Morogoro. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 24,
2017 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es
Salaam.

Kaimu
Mtendaji wa Kampuni Tanzu ya Mkulazi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya
NSSF & PPF, Bw. Nicander Kileo (kushoto) na Kamishna Jenerali wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) kwa pamoja wakisaini Mkataba wa
Makubaliano(Memorundum of Understanding) kati ya Jeshi la Magereza na
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa
kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza
Mbigiri – Morogoro. Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika leo februari
24, Jijini Dar es Salaam.

Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) na Kaimu Mtendaji wa
Kampuni Tanzu ya Mkulazi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF &
PPF, Bw. Nicander Kileo(kushoto)wakionesha nyaraka mbalimbali baada ya
hafla fupi ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la
Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika
ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari
cha Gereza Mbigiri – Morogoro.

Maafisa
Waandamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF
wakifuatilia hafla ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano hayo kama
inavyoonekana katika picha.

Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF, Bw. William Erio akizungumza
katika hafla fupi ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya
Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika
ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari
cha Gereza Mbigiri – Morogoro.

Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia uwekaji saini wa Mkataba
wa Makubaliano hayo kama inavyoonekana katika picha.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF,
Prof. Godius Kahyarara akizungumza katika hafla fupi ya uwekaji saini
wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi
ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha
miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro.

Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Maafisa Waandandamizi wa Jeshi la Magereza(waliosimama) mara
baada ya hafla ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano hayo(wa pili
kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF, Bw.
William Erio(wa pili toka kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
0 Comments