Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp
amewapa matumaini mapya mashabiki wa timu hiyo kuwa katika michezo 14
ambayo imesalia kabla ya kumaliza msimu watashinda michezo yote hali
ambayo itaiweka klabu hiyo katika nafasi nzuri kama ni kushinda ubingwa
au kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Liverpool kwa sasa ipo nafasi ya tano
ikiwa na alama 46, alama 13 nyuma ya viongozi wa ligi Chelsea, lakini
Klopp amesema katika soka kila jambo linawezekana na imani yake ni
kushinda michezo yote 14 ambayo ipo mbele yao.
“Katika ndoto zangu tunaweza
kushinda michezo 14, najua inaweza kupokelewa tofauti lakini siwezi
kubadili ndoto zangu na hilo ndilo ninalolifanyia kazi na baada ya
michezo 14 utakuwa muda wa kuangalia ni nini tumejifunza kutoka kwa
wengine alafu tutafanya maamuzi ambayo yanaweza kutusaidia kwa msimu
ujao,” alisema Klopp.
Ndoto ya Klopp kushinda michezo 14
itaanza kupimwa leo usiku wakati Liverpool itakapokuwa mwenyeji wa
Tottenham kwenye uwanja wa Anfield, Tottenham wao wana alama 50 na
wakiwa nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

0 Comments