Dada Neema Mwita Wambura (32) akizungunza na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu
akimshukuru kwa msaada aliompatia wa kufanyiwa tena uchunguzi wa afya
yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia Rais Dkt. Magufuli
ameahidi kumpatia hifadhi mama huyo pamoja na watoto wake watatu ambao
kwa sasa wapo Bunda mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpatia msaada
Dada huyo kiasi cha Shilingi laki tano. Dada Neema Mwita Wambura
aliungua vibaya mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa unachemka
jikoni na mume wake katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara.
Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) ambaye amempa hifadhi
Neema Mwita Wambura nyumbani kwake Tandika Davis Corner akiomba dua
kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kupitia njia ya Simu kumshukuru mara baada ya kuzungumza naye
kuhusiana na kumsaidia Dada Neema Mwita Wambura (32). Rais Dkt. Magufuli
amempongeza Mama huyo Mjane ambaye ameonesha moyo wa kizalendo na kumpa
hifadhi Dada huyo aliyemwagiwa uji wa moto na mumewe katika kijiji cha
Kyagata, Tarime mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpa Mjane huyo
kiasi cha Shilingi laki tano.
Dada Neema Mwita Wambura (32) wakwanza kulia akiwa pamoja na
Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) wakiwa ndani ya gari mara baada
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
kumsaidaia ili aweze kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimpokea Dada Neema
Mwita Wambura (32) na kuanza mara moja kumfanyia tena uchunguzi wa afya
yake katika majeraha aliyoyapata mara baada ya kumwagiwa uji wa moto
uliokuwa ukichemka jikoni kitendo kilichofanywa na mume wake.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa
Lawrence Museru akimjulia hali Dada Neema Mwita Wambura (32) mara baada
ya kufikishwa tena hospitalini hapo. Dada Neema Mwita alifanyiwa
upasuaji mara nne katika siku za nyuma hospitalini hapo Muhimbili ili
kutibu majeraha yake hayo ya moto.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura na Ajali katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga akizungumza kuhusu hali ya
mgonjwa Dada Neema Mwita Wambura (32) aliyefikishwa tena katika
Hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi wa Afya yake.
Dada Neema Mwita Wambura (32) akiwa katika hali ya majonzi
kufatia majeraha makubwa mwilini mwake kufatia kumwagiwa uji wa moto na
mume wake mkoani Mara.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa ngozi kutoka Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili Dkt. Ibrahim Mkoma akizungumzia historia ya mgonjwa huyo
ambaye yeye pamoja na jopo la madaktari bingwa walimfanyia upasuaji ili
kutibu majeraha yake ya ngozi katika kipindi cha nyuma. PICHA NA IKULU









0 Comments