Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro Urich Matei (katikati) akiwa na viongozi wengine wa
majeshi ya magereza Mkoani humo wakitembea kwa ukakamavu wakati wa mazoezi ya
pamoja Februari 11 mwaka huu.
Mbunge
wa Morogoro Mjini Mhe.
Mohamed Abood Azizi (mwenye mavazi mekundu mbele) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa
wa Morogoro Dkt Kebwe (kushoto kwake) wakiongoza
mamia ya watu waliofiki kushiriki mazoezi ya mwili.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro (mwenye Truck rangi
ya bluu) akiwa katika mazoezi mepesi Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro siku ya Jumamosi ya Februari 11,2017. Kushoto kwake ni Mbunge
wa jimbo la Morogoro mjini Mhe.
Mohamed Abood Azizi, na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo.
...............................................................................................
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Dkt. Steven Kebwe amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhandisi Dkt. John
Ndunguru kuratibu vikundi vingine vya mazoezi na wananchi wengine Mkoani
Morogoro kujiunga na mazoezi ya viungo yanayofanyika kila Jumamosi ya pili ya kila
mwezi kwa lengo la kuimarisha Afya zao.
Dkt. Kebwe ametoa agizo
hilo mwishoni mwa wiki hii muda mfupi kabla Mkuu huyo kuongoa mamia ya watu
kutoka Taasisi za Umma na watu binafsi waliofika kushiriki mazoezi hayo na Mkuu
huyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali la kufanya pamoja mazoezi ili
kulinda Afya zao.
Dkt. Kebwe alisema,
mazoezi hayo hayakuanzishwa kwa ajili ya watumishi wa umma pekee bali kwa ajili
ya wananchi wote na lengo lake ni kupunguza magonjwa yasiyoambukizwa kwa
wanannchi wote na kumuagiza Katibu
Tawala wa Mkoa huo kuendelea kuratibu ili kuvipata vikundi au watu wengine
kujiunga na mazoezi hayo.
“Lakini RAS, suala hili
lifuatiliwe, kwa mujibu wa waraka kutoka kwa Makamu wa Rais Makatibu Tawala wa
Mikoa ndio wenyeviti wa shughuli hii ya michezo kwa Mkoa mzima”, Dkt. Kebwe
alisema. “kwa hiyo Mwenyekiti, tafadhali simamia ili watu wengine waendelee
kuratibiwa kwa kuwa mazoezi haya siyo kwa ajili ya watumishi wa umma tu bali
kwa watu wote” alisisitiza
Pamoja na wito huo Mkuu
huyo wa Mkoa wa Morogoro ameitahadhalisha jamii kuwa magonjwa yasiyoambukizwa
yanapanda kwa kasi hapa nchini na dawa pekee ya kutibu magonjwa hayo ni kufanya
mazoezi. Ameyataja magonjwa hayo kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, kiharusi,
magonjwa ya moyo saratani n.k.
Awali kabla ya kuanza
mazoezi hayo Mkuu wa Mkoa aliwashukuru wote waliofika kushiriki michezo na
kwamba ameridhika na mwitikio huo huku akitaka watu wengi zaidi waendelee
kuitikia wito wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan wa kuungana kufanya mazoezi ya pamoja kila Jumamosi ya pili ya
kila mwezi.
Mazoezi hayo yaliyoanzia
katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kuishia Uwanja wa Jamhuri uliopo
katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoroa yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali
wa Mkoa huo akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa Mhandisi Daktari John Nunguru, Kamanda
wa Polisi wa Mkoa Urich Onesphori Matei,
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo na Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mhe.
Mohamed Abood Azizi.



0 Comments