Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiongea jambo wakati akiwaeleza
wananchi na wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Nyamagongo Wilaya ya
Rorya kuhusu utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya III. Shule hiyo ni miongoni
mwa maeneo ambayo yatafikiwa katika mradi wa REA awamu ya Tatu. Wengine
wanaofuatilia ni Meneja wa TANESCO
Kanda ya Ziwa Mhandisi Amos
Maganga, (katikati) Meneja wa TANESCO
Wilaya ya Rorya, Sospeter Kswahili (wa kwanza kulia). Wengine ni Mtaalam
kutoka Wakala wa Nishati Vijijini Mhandisi Emmanuel Yesaya na Mkandarasi wa
Kampuni ya Angelica International.
Afisa Uhusiano na
Huduma za Jamii kwa Wateja kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), James Vesso, akitoa elimu kuhusu Kifaa cha
Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa Kijiji cha Muriaza Kata ya Muriaza Wilaya
ya Butiama wakati wa Ziara ya Waziri wa
Nishati na Madini kijijini hapo. Kifaa hicho hakihitaji mtandao wa umeme katika
nyumba.
Meneja
wa TANESCO Kanda ya Ziwa Mhandisi Amos Maganga, akizungumza jambo
wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini wananchi wa Nyamagongo
ambapo Waziri na wataalam wa REA na TANESCO wameeleza kuhusu utekelezaji
wa REa Awamu ya Pili na ya Tatu. Wengine ni Mameneja wa TANESCO, Wilaya ya Rorya na Mkoa wa Mara, na Wataalam
kutoka REA na TANESCO.
Mkuu wa Wilaya
ya Rorya, Saimon Chacha na viongozi wa Mkoa, wakimkaribisha Waziri wa Nishati
na Madini Profesa Sospeter Muhongo
(kulia) wilayani humo kwa ajili ya ziara ya kukagua miradi ya REA awamu ya II
na kueleza mipango ya Serikali kuhusu utekelezaji wa REA Awamu ya Tatu.

Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mhandisi Hamis Komba, akiwaeleza wachimbaji
wadogo kuhusu shirika hilo kuridhia kutoa sehemu ya eneo lake la Buhemba kwa
ajili ya wachimbaji kufanya shughuli za uchimbaji madini.
Mtendaji
Kata wa Mirwa, Neema Philipo,akisoma majina ya vikundi vya wachimbaji wadogo
ambavyo vitapewa sehemu ya eneo la STAMICO, Buhemba. Wengine wanaofuatilia ni
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kushoto), Kaimu
Mtendaji Mkuu wa STAMICO, Mhandisi Hamis Komba, (wa kwanza kushoto) Kamishna
Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Mashariki, Mhandisi Juma Sementa na
Watendaji kutoka STAMICO na wachimbaji wadogo.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akitoa rambirambi kwa baadhi ya
wazazi ambao mmoja wa wachimbaji wadogo alifariki katika ajali ya kifusi
iliyotokea katika mgodi eneo la Buhemba,
Mkoani Mara.
Sehemu
ya wananchi wa wananfunzi katika eneo la
Nyamagongo Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara wakifuatilia mkutano wa Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, hayupo pichani
Naibu
Mhariri wa Gazeti la Jamhuri Jackton Manyerere (wa pili kulia) akiongea jambo
wakati Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa heshima katika Kaburi la Baba Mzazi
wa Manyerere., Jakcton Nyambereka Nyerere aliyefariki dunia tarehe 19/2/2017/.
Wa kwanza kulia ni Mhariri wa gazeti la Mtanzania Kulwa Keredia. Kushoto ni
baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari. Waziri alifika kuhani
msiba wa wahariri hao Manyerere na Keredia wakati wa ziara yake Wilayani
Butiama.








0 Comments