Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Andrew Kabeho
akimpima mapigo ya moyo Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
Mohamed Kiganja aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima
magonjwa ya moyo. JKCI inashiriki katika kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi
na kupima afya bila malipo iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee
na Watoto na kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Baadhi ya wanakamati wa kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na
kupima afya iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na
kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma wakitayarisha fomu za kujaza
wananchi watakaofika katika uwanja huo kwa ajili ya kupima afya zao bila
malipo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akimpima ugonjwa wa kisukari Agnes Luberi
aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo
bila malipo huku wanafunzi wanaosomea kozi ya udaktari katika Chuo kikuu cha
Dodoma wakiangalia. Zaidi ya wananchi 170 walifika katika banda hilo kwa siku
ya kwanza ya upimaji kwa ajili ya kupima afya zao ili kujuwa kama
wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo au la.
Waandishi wa Habari wakichukua matukio mbalimbali katika banda la
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo
kwa siku mbili iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia , Wazee na Watoto inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Dodoma wakiwa katika mstari wa
kusubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya
kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa siku mbili iliyoandaliwa
na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto na kufanyika
katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Daktari Bingwa
wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro
Pallangyo akimweleze madhara ya magonjwa ya moyo mwananchi aliyefika katika
banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo bila malipo ili
aweze kujuwa kama anasumbuliwa na magonjwa ya moyo au la.
Picha na Anna
Nkinda – JKCI







0 Comments