
Mchezaji
wa timu za Kisiju Pwani kulia wa kushoto akijaribu kumtoa beki wa timu
ya Lukanga Fc wakati wa kivumbi cha mashindano ya ULEGA CUP hatua ya
nusu fainai iliyopigwa kwenye uwanja wa shule ya msingi mkuranga,Kisiju
waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutinga hatua ya fainali.

Mchezaji wa timu ya Lukanga Fc wa kushoto akiwa katika harakati zake za
kuwapita wachezaji wa timu ya Kisiju Pwani katika mchezo wa kwanza wa
hatua ya nusu fainali ya michuano ya ULEGA CUP kwenye uwanja wa shule ya
msingi Mkuranga.

Wachezaji wa timu zote mbili wakiwa uwanjani kuisakata kabumbu katika mchezo wa nusu fainali hiyo.
(PICHA NA VICTOR MASANGU)
...............................................
NA VICTOR MASANGU, MKURANGA
TIMU
mbili za soka za Kisiju Pwani pamoja na Tengelea Fc zimefanikiwa kukata
tiketi ya kutinga katika hatua ya fainali baada ya kuibuka na na
ushindi katika michezo miwili waliyoicheza hatua ya nusu fainali kwenye
kinyang’anyiro cha michuano ya ‘ULEGA CUP 2016-2017 ’ kwenye uwanja
wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani.
Michuano
hiyo ambayo imeandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah Ulega
kwa lengo la kuweza kuibua na kukuza vipaji vya wachezaji mchezo wa
kambumbu ambao walishirikishwa kutoka katika kata zote 25 zilizopo
katika jimbo hilo.
Katiha
mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza iliweza kuzikutanisha timu ya
Kisiju Pwani ambao walimenyana na majirani zao wa karibu timu ya
Lukanga Fc ambapo timu ya Kisiju ndio iliyoweza kuchupa fainali baada
ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao.
Bao
la washindi katika mtanange huo liliwekwa kimiani na mshambuliaji wao
wa kutumainiwa Mudy Mbete kunako katika dakika ya 71 baada ya kuachia
shuti kali lilizozama moja kwa moja langoni na kumwacha mlinda mlango wa
timu ya Lukanga Fc amebaki mdomo wazi.
Mchezo
mwingi wa hatua ya nusu fainali ya pili ambao ulikuwa unasubiriwa kwa
hamu na shauku kubwa na wadau na mashabiki wa mchezo huo timu ya
ulizikutanisha timu ya Tengelea Fc ambao walicheza na Mwandege ambapo
Tengelea waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililopachikwa na mchezaji
Andrwe Joseph kunako katika dakika ya 80 na kufanikiwa kupata nafasi ya
kucheza hatua ya fainali.
Kwa
matokeo hayo timu ya Kisiju Pwani pamoja na timu ya Tengelea Fc ambao
ndio wameweza kushinda katika michezo yao ya nusu fainali watakutana uso
kwa uso katika mchezo wa fainali unaotarajiwa kufanyika machi 5 mwaka
huu kwenye dimba la shule ya msingi Mkuranga.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdlah Ulega ambaye ndio
mwandaaji wa mashindano hayo ya soka alisema kwamba nia yake kubwa ni
kuunda timu ya Jimbo ambayo itakuwa ikishiruki katika ligi mbali mbali
na ndoto yake kubwa ni kuhakikisha nashirikina na wadau wa soka ili kuwa
na kikosi kizuri amabcho kitaweza kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara
katika siku za usoni.
0 Comments