Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya
Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo
yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza
na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Makumbusho ya
Taifa Profesa Audax Mabulla akizungumza wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki
ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho
hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya
kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini
Tanzania Mossa Farharng (wa pili kutoka kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye (hayupo pichani)
wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni
cha Iran Ali Bagheri na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce
Fissoo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Nape Moses Nnauye akicheza Bao na Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Jadi
Tanzania Bw. Mohamed Kazingumbe (kulia) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki
ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho
hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya
kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Baadhi ya Wasanii kutoka Iran wakitumbuiza
muziki wa Ala wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya
Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli
mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza
Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Nape Moses Nnauye akiangalia moja ya vitabu vyenye maneno ya Kishiraz wakati wa
kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo
jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa
Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila
na desturi zake”. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni
Bibi. Lilian Beleko, Balozi wa Iran nchini Mossa Farharng na Mkurugenzi wa
Kituo cha Utamaduni cha Iran Ali Bagheri.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Nape Moses Nnauye akisikiliza maelezo kuhusu michoro ya Kiutamaduni ya Iran
wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania
leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano
wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na
Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Nape Moses Nnauye akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Utamaduni wa Bodi ya
Filamu Tanzania Bw. Benson Mkenda alipotembelea meza ya Bodi hiyo wakati wa
kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo
jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa
Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila
na desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Nape Moses Nnauye akifurahia jambo mara baada ya kupata maelezo ya namna ya
kufanya marekebisho ya Vitabu kutoka kwa Ali Navidogooe Shiraz wakati wa kilele
cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar
es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni
ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi
zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Nape Moses Nnauye akipiga Gitaa
lililotengenezwa na Msaanii wa Uchoraji na Uchongaji Bw. Washington
Steven Masanja (kushoto) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni
baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam.Maonyesho hayo yalikuwa na
kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na
kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”. Kushoto kwa Waziri ni
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Wasanii wa Mashairi Bw. Issa Amiri Kilimo aka.
Kijoka Kidogo na Mwajuma Seleman Yombe wakiimba shairi kwa njia ya majibizano
ikiwa ni kujibu shairi la Siri la mtunzi Haji Myaka bin Haji la mwaka 1405 le
jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina
ya Shiraz na Tanzania.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini
Tanzania Mossa Farharng akimkabidhi zawadi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Nape Moses Nnauye wakati wa
kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho
ya Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Nape Moses Nnauye akifurahia jambo na Balozi
wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng wakati wa kilele cha Wiki
ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini
Dar es Salaam leo.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng na baadhi ya
viongozi kutoka taasisi za Serikali na ubalozi wa Iran wakati wa kilele cha
Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
jijini Dar es Salaam leo.
Picha na: Frank Shija
– MAELEZO.
....................................................
Na Shamimu
Nyaki-WHUSM.
Serikali chini ya Wizara ya Hbari Utamaduni
Sanaa na Michezo inaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa Utamaduni wa
Mtanzania unakuwa sehemu ya muhimu ya kivutio cha Utalii ili kutengeneza ajira
na kuingizia Serikali mapato.
Hayo yamesemwa na
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipokuwa
anafungwa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi yaliyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa madhimisho haya yanaimarisha undugu wa
damu wa kiuchumi na kiutamaduni ulioachwa na wahenga.
“Maadhimisho ya wiki
ya Utamaduni wa Shirazi ni fursa pekee ya kujifunza kutoka kwa kwa wairani
namna ya kukuza ,kulinda na kuendeleza Utamaduni,Sanaa,Filamu,Mila na Desturi
zetu”Alisema Waziri Nape.
Aidha ameongeza kuwa Wizara
yake itaweza kufanikisha shughuli za
Utamaduni na kuziendeleza kwa
kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya
ya nchi kama ilivyofanyika katika
maadhimisho ya mwaka huu kwani yanatangaza vikundi vya Sanaa na Wasanii.
Kwa upande wa wake
Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Irani hapa nchini Bw.Ally Baghari amesema kuwa
ushirikiano wa Kiutamaduni baina ya Tanzania na Irani umeongeza mafanikio ya
kiuchumi na kijamii katika nchi hizo hasa kupitia ubadilishanaji wa Utamaduni
tangu enzi za ukoloni.
“Tumejifunza
utamaduni wa kitanzania kupitia
maadhimisho haya na tunaamini watanzania pia wamejifunza utamaduni wa Irani
ambao umesaidia kuimarisha ushirikiano wetu”Alisema Bw Baghari.
Maadhimisho hayo
yaliyokuwa na kauli mbiu “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza
na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.














0 Comments