Mwanzilishi wa Saccos cha Wanawake Wajasiriamali
Tanzania (TASWE) Dkt. Anna Matindi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuhusu
Mkutano wa Kimataifa wa Vijana kutoka Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi, leo
Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu
wa Chama cha Vijana Wajasiriamali – Taswe Bi. Adelaida Ngowi. Mkutano huo
unatarijiwa kufanyika tarehe 24 Machi, 2017 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa
Osterbey huku kauli mbiu yake ikiwa ni “Badilisha Mtazamo wa Vijana wajielekeze
katika Sekta Binafsi” .
Mwanzilishi wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha
Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TASWE) Dkt. Anna Matindi akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Vijana kutoka Vyuo
Vikuu vya ndani na nje ya nchi, leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu wa Chama cha Vijana
Wajasiriamali – Taswe Bi. Adelaida Ngowi, Mwanachama wa Taswe Bi. Grace Kimaro.
Mkutano huo unatarijiwa kufanyika tarehe 24 Machi, 2017 katika ukumbi wa
Kardinali Rugambwa Osterbey huku kauli mbiu yake ikiwa ni “Badilisha Mtazamo wa
Vijana wajielekeze katika Sekta Binafsi” .
Mwanachama wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TASWE) Bibi. Leah Paul Dennis akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Vijana kutoka Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi, leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu wa Chama cha Vijana Wajasiriamali – Taswe Bi. Adelaida Ngowi, Mwanzilishi wa Chama hicho Bibi.Anna Matinde na Bi. Grace Kimaro. Mkutano huo unatarijiwa kufanyika tarehe 24 Machi, 2017 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa Osterbey huku kauli mbiu yake ikiwa ni “Badilisha Mtazamo wa Vijana wajielekeze katika Sekta Binafsi”
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.
.....................................................................
Na: Frank Shija - MAELEZO
VIJANA zaidi ya 1000 kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali
vya ndani na nje ya nchi kukutanishwa jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa
Kimataifa utakaofanyika tarehe 24 Machi 2017 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa, Osterbay
Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa na Mwanzilishi wa Chama cha
Kuweka na Kukopa cha Wajasiriamali Wanawake Tanzania (TASWE) Anna Matinde
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo leo jijini Dar es
Salaam.
Bibi. Matinde amesema kuwa TASWE kwa kushirikina
na Kikundi cha Kwaya ya Remnant Generation wameandaa Mkutano maalum kwa ajili
ya vijana wa Vyuo Vikuu kwa leongo la kuwajengea uywezo na kuwabadilisha fikra
ili watambuefursa zilizopo katika Sekta binafsi.
“Tarehe 24 mwezi Machi kutakuwa na Mkutano mkubwa
wa Kimataifa ambapo vijana kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali watashiriki na
kujengewa uwezo”. Alisema Matinde.
Kwa upande wake
Katibu wa Vijana Wajasiriamali kutoka TASWE amaesema kuwa lengo kubwa la
mkutano huo ni kuwakutanisha vijana na kuwapa elimu itakayowabadilisha mitazamo
yenye lengo la kuwafanya wafikirie kujikita katika Sekta binafsi badala ya
kutegemea kuajiriwa pindi watakapomaliza masomo yao ya elimu za juu.
Aliongeza sambamba na
kubadilisha mitazamo yao mkutano huo utasaidia kuwaondolea msongo wa mawazo
utokanao na ukosefu wa ajira pamoja na ukweli kwamba wahitimu wamekuwa
wakiongezeka siku hadi siku huku ajira zikikua kwa kasi ndogo.
“Takribani Vijana
1200 kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi
wanatarajia kukutana ikiwa lengo kubwa ni kuwasaidia vijana hao na kutambua
kuwa ujasiriamali ni sehemu ya ajira”, alisisitiza Bi. Adelaida.
Mkutano huo wa
Kimataifa wa Vijana unaandaliwa kwa ushirikiano baina ya Chama cha Kuweka na
Kukopa cha Wajasiriamali Wanawake Tanzania (TASWE) na Kikundi cha Wanakwaya cha Remnant Generation
kinachojali wahitaji kwa kusaidia mahitaji ya. Kauli mbiu ya mkutano huo ni
“Badilisha Mtazamo wa Vijana wajielekeze katika Sekta Binafsi”.




0 Comments