Random Posts

VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA NI YETU SOTE - RAIS MAGUFULI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kumwapisha Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo na Kamishina wa Magereza leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo akiweka saini katika hati ya kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (CDF) leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli  akiweka saini katika hati ya kiapo cha utii wakati wa hafla ya kumwapisha Mkuu wa Jeshi la Wanchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo leo jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Mkuu mpya wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo leo jijini Dar es Salaam.
 Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Meja Jenerali James M. Mwakibolwa akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major Jenerali James M. Mwakibolwa akiweka saini katika hati ya kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (CDF) leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli  akiweka saini katika hati ya kiapo cha utii wakati wa hafla ya kumwapisha Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Meja Jenerali James M. Mwakibolwa leo jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli  akimkabidhi vutendea kazi Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major Jenerali James M. Mwakibolwayo  wakati wa hafla ya kuwapisha wateule hao leo jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa wakati wa hafla ya kuwapisha wateule hao leo jijini Dar es Salaam.
 Balozi Paul Mella ambaye ataiwakilisha nchi ya Tanzania nchini katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Balozi Samweli William Shelukindo ambaye anakwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Ufaransa akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Nyakimura Mathias Mhoji akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna Robert Boaz Mikomangwa akila kiapo cha utii mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Inspekta Jenerali Ernest Mangu katika hafla ya kuwaapisha baadhi ya viongozi walioteuliwa na Mhe. Rais kushika nyazifa mbalimbali leo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance S. Mabeyo ( kulia) mara baada ya hafla ya kumuapisha leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mnadhimu wa Jeshi hilo Meja Jenerali James Mwakibolwa, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohamed Shein na Waziri Mkuu wa Kassim Majali.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance S. Mabeyo akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyage wakati wa hafla ya kuapishwa kwake leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania wakati wa hafla ya kuwaapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Mabalozi pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma leo jijini Dar es Salaam.


Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
............................................................

Beatrice Lyimo - MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa vyombo vya ulinzi kuendeleza vita dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya  kuwaapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali James Aloyce Mwakibolwa.

Rais amesema kuwa kitendo cha Mkuu wa Jeshi la Polisi Ernest Mangu kuwasimamisha baadhi ya watendaji kazi wake kimeipa heshima jeshi la polisi nchini.

“Madawa ya Kulevya yanapoteza nguvu kazi za watanzania hasa vijana, hivyo hii kazi si ya mtu mmoja ni ya wanzania wote kushirikiana kwa pamoja katika kupambana na jambo hili kwa manufaa ya nchi” alifafanua Rais Magufuli.

Mbali na hayo alisema kuwa, katika mapambano vipo vikwazo kadha vitakavyojitokeza hivyo watanzania wanabudi kuungana kwa pamoja dhidi ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya.

Katika hatua hiyo Rais Magufuli alisema kuwa kwa sasa nchi inavyoelekea katika uchumi wa kati kupitia viwanda, amelitaka Jeshi la Ulinzi nchini kusimamia na kujenga nchi ya viwanda kwa vitendo.

“haiwezekana Tanzania ya leo bado inaagiza sare kutoka china,wakati nchi yetu ina wakulima wazuri wa pamba, hivyo vyombo vya ulinzi mnatakiwa kujipanga katika hili, mkiamuua kuzungumza na baadhi ya viwanda na kuwapa vipimo na ubora wa nguo, rangi watatengeneza. ”alisema Rais Magufuli.

Alisema kuwa si kila kitu lazima kununua kutoka nje, ni lazima kujipanga kwa kuhakikisha dhana ya viwanda inaanzia jeshini.

“Tubadilike tutengeneze Tanzania kwanza, maslahi ya nchi yapewe kipaumbele, rasilimali zilizopo zitumike kwa manufaa ya nchi” alisisitiza Rais Magufuli.

Katika hatua hiyo Rais Magufuli alitoa wito kwa majeshi nchini kutoa ushirikiano kwa wateule, kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa manufaa ya nchi na askari wengine.

Kwa upande wake Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ali Shein alisema kuwa jeshi la Tanzania linasifa kubwa ndani na nje ya nchi hivyo anaamini wateule wapya watafanya kazi hiyo kwa umahiri mkubwa.

Naye Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange alisema kuwa katika kipindi cha uongozi wake, ajali ya milipuko ya mabomu yaliyotokea Mbagala na Gongola mboto ndio kilikuwa kipindi kigumu kwake kwani watu waliumia na mali za wananchi na za jeshi zilipotea.

Wakati huo Jenerali Mkuu wa Majeshi aliyeapishwa leo Venance Mabeyo ameahidi kuendeleza na kuimarisha ulinzi wa taifa la Tanzania pale ambapo Jenerali Mstaafu Mwamunyange alipoishia na kama ilivyo majukumu ya jeshi kimsingi.

Rais Magufuli pia aliwaapisha Kamishina Jenerali wa Magereza Dkt Juma Alli Malewa ambaye alikuwa Kamishina wa Sheria na Uendeshaji wa Taifa la Magereza.

Wengine ni Balozi Paul Mella ambaye ataiwakilisha nchi ya Tanzania nchini katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Balozi Samweli William Shelukindo ambaye anakwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Ufaransa pamoja na Nyakimura Mathias Mhoji ambaye amekuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma.

Naye Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu amemuapisha Kamishina wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

Post a Comment

0 Comments